Monday, July 28, 2014

WIZI WA MABENK TANZANIA-KAMISHNA KOVA AUNGURUMA LEO.ATOA PIA NENO LAKE KUELEKEA SIKU YA IDDI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivWEkNwWZDu_fj7GHt8rR9Pq2hyphenhyphenwv2DUwqCYVIIJDR91N8hje08ykCCC-yrBbp-82rL0NcVK9E_KB7ev0nRBUN11SMsJPqfnRm85-p5DpZ258Vy_1Gne4b1K0edRO6AqklZZdCbU8-ljBj/s1600/3.jpgNa Karoli Vinsent
  
         JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam limefichua Siri ya kuongezeka Vitendo vya  ujambazi katika maBenki mbalimbali hapa nchini na kusema vitendo hivyo vinasababishwa na Wamiliki wa Mabenki hayo kulipuuza Jeshi la polisi,

          Kauli hiyo ya Jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam imekuja  SIKU moja kupita baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi kuvamia katika Benki ya Stanbic tawi la Kariakoo liloko mtaa wa Swahili na kukomba mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo Mteja,

       Kauli hiyo imetolewa Mda huu na Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dar Es Salaam,Suleiman Kova wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam,ambapo alisema watu wanaochangia Vitendo hivyo vya Ujambazi kuzidi kuongezeka katika Mabenki mbalimbali hapa nchini ni Wamiliki wa Mabenki kupuuza ushauri wa Jeshi la Polisi ,


        Uliowataka waache kutumia walinzi wa Makampuni Binafsi peke yake,watumia na Walinzi kutoka Jeshi la polisi.

       “Nataka niwambie waandishi hivi vitendo vya Uvamizi kwenye mabenki  viemtokana na wamiliki wamabenki hayo kupuuza ushauri wetu uliowataka kwenyes shuhuri za Ulinzi kwenye mabenki watumike Polisi tu,lakini wao wakapuuza,ukitaka kuamini Nenda kwenye Mabenki yanayolindwa na Polisi kama utaona kama kunauvamini wowote uonotokea,kwasababu majambazi hao wanashindwa kuvamia kutokana na umakini wa Jeshi la Polisi”alisema Kova

          Kamishna Kova,alisema kwa sasa la polisi limejipanga kuongea na Benki kuu(BOT) ambaye ni kiongozi wa Benki zote hapa nchini na kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo la Mabenki Mengine kupuuza ushauri huo wa Jeshi la polisi.

         Vilevile jeshi hilo la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Limeeanza msako kali wa kuwatafuta Majambazi watano waliovamia Jana kwenye Beki ya Stabic Tawi la Kariakoo lilioko mtaa wa Shwahili majira ya mchana.

         Kwa Mujibu wa Kamishna Kova alisema watu wa tatu kati yao waliingia ndani ya Benki hiyo wakiwa na Mifuko Mikubwa wakijifanya ni wateja wanapeleka Fedha nyingi katika Benki hiyo,watu hao walipoingia ndani walianza kuwalazimisha kuvuka wigo wa wateja wa kwaida na kutaka kuingia kwa nguvu kupora Fedha.

          Ambapo Benki hiyo ya Stabinc ina mitambo ya Aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vingora vya Tahadhari,ikasaidia kwa majambazi hao kushindwa kuingia ndani kuiba pesa za Benki hiyo kutokana na Vingora hivyo kupiga kelele na kuanza kuwapa uwoga majambazi hao ,ambapo walifanikiwa kuiba pesa za mteja mmoja ambae alikuwa anataka kuweka pesa kwenye benki hiyo,

          Kova alisema Majambazi hao walipotoka nje ya Benki hiyo walipiga Risasi Juu ili kuwapa Hofu wananchi walikuwa Nje ya Benki hiyo,ambapo kwa Mujibu wa Kamishna Kova anasema bado wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.

         Katika Hatua nyingine Jeshi hilo la polisi Limejipanga ipasavyo kwenye sikuku ya IDD El Haji 2014,ambapo jehi hilo limesema limepanga kushikirikiana na Vyombo mbalimbali vya ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi  cha Zima Moto na Uokoaji,Kampuni Binafsi za ulinzi lengo ni kuhakikisha wananchi wanafurahia kwa utulivu na amani kwenye sikuku hii.
 

No comments: