Friday, August 29, 2014

BREAKING NEWZ--HUZUNI YATANDA MBEYA,AJALI MBAYA TENA,KUMI WAFARIKI HAPO HAPO

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa watu kumi wakiwemo watoto wawili, 
wamefariki dunia papo hapo na wengine 
saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali 
iliyohusisha magari mawili.

Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria 
maarufu daladala lenye namba za usajili T 
237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa 
aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 
CSV.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo 

wamesema ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea 
Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso 
lililokuwa likiingia barabarani.

Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu 
hayajaweza kupatikana mara moja kutokana 
na kuwa katika hali mbaya huku dereva 
wa Fuso akitokomea  baada ya tukio.

No comments: