Friday, August 29, 2014

UCHAGUZI CHADEMA MOTO--HUYU NDIYE MGOMBEA WA UMAKAMU WA MWENYEKITI

Na karoli Vinsent
  
     MWANASIASA, wakili wa Mahakama Kuu, Mwanazuoni na mtetezi wa haki za Waislamu nchini, Prof. Abdallah Safari, amejitosa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Taarifa zilizothibitishwa na Prof. Safari mwenyewe zinasema, mwanasiasa huyo mashuhuri nchini anatarajiwa kuchukua fomu wakati wowote kati ya leo na kesho  kuwania moja ya nafasi za juu za uongozi. Ambapo Atawania umakamu mwenyekiti Tanzania Bara.

        Akizungumza na Mtandao mmoja wa Masuala ya kisiasa Nchini muda mfupi uliyopita, Prof. Safari amesema, ameamua kugombea nafasi hiyo ili kutimiza adhima yake ya kuimarisha upinzani na kuhakikisha chama tawala kinaondoka madarakani.

"Nilijiunga na Chadema nikitokea Chama cha Wananchi (CUF). Kule niligombea nafasi ya uenyekiti. Kwa bahati mbaya sana, sikufanikiwa kushinda. Sasa nimejiunga na Chadema na hivyo nataka kile ambacho ningekifanya CUF, nikifanye Chadema," ameeleza.


           Prof. Safari vilevile ambaye ni mwandishi wa Vitabu mbalimbali nchini ikwemo Riwaya ya Nyoka mdimu na nyingine alijiunga na Chadema miaka mitatu iliyopita, ambako mwenyekiti wake wa sasa, Freeman Mbowe alimteuwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

          Tangu kujiunga na Chadema, mwanasiasa huyo amekisaidia chama hicho katika maeneo mbalimbali, lakini kubwa linalotajwa ni kuzima hoja za udini ambazo Chadema imekuwa ikipakaziwa na wapinzani wake wa kisiasa.

    Kuibuka kwa Profesa Safari kwenye Kinyang’anyiro hicho kunazidi kuongeza idadi ya wagombea ndani ya chama hicho katika nafasi za juu ambapo jana mwenyekiti wa chama hicho FREMAN MBOWE amechukua fomu ya kutetea nafasi yake.

Mbowe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai,jana wakati wa Mkutano na waandishi wa habari alithibitisha Rasmi kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya juu ya chama hicho ambacho ni kikuu cha upinzani nchini kwa sasa,\
Ambapo Mbowe alianza kwa kueleza sababu mbalimbali alizodai zimemshangaza kuona ni kwa nini awe yeye licha ya chama kuwa na watu wengi wenye uzoefu na weledi.

Alisema kuwa ameshangazwa na namna makundi mbalimbali yalivyojitokeza na kumtaka agombee ilhali wapenda majungu wanadai amewapanga wakati hakuwa na mpango wa kugombea tena nafasi hiyo.
“Mimi sikuwaza kugombea na niliwahi kukataa mara kadhaa. Nilikuwa nawaza kumpata ‘Mnyamwezi’ mwingine mwaminfu wa kumkabidhi kijiti lakini Kamati Kuu iliyokaa hivi karibuni ilinikatalia kufanya hivyo na mara kadhaa iliniomba nigombee tena,”alisema Mbowe.

  Alisema hadi kufikia jana, alikuwa hajachukua fomu na kwamba alipanga siku ya leo awe safarini kuelekea nchini Uingereza.
Mbowe alijigamba kuwa kutokuwa na uelewa na weledi katika uongozi, kuliwafanya watu wengine kupotelea njiani kwa kutojua.

Alisema kuwa kuna wanaotumika na kuna walioishiwa na nguvu na hata wengine kupata fedha kuhakikisha malengo ya kuvuruga chama yanatimia lakini yeye alipambana hadi CHADEMA ikasonga mbele.
“Sikuwahi kuomba hata mara moja kugombea nafasi hii katika vipindi vyangu vitatu. Mwaka 2004, niliombwa na aliyekuwa Mwenyekiti Bob 

Makani, nikakataa lakini jopo la Wazee liliniomba, nikakubali.
“Mwaka 2005, pia sikuomba kugombea urais, na nafasi hiyo ilikuwa igombewe na Prof. Mwesiga Baregu ambaye mwishoni alijitoa na nikaombwa nigombee mimi,”alisema.

Kwa mujibu wa Mbowe, mwaka 2009, aliombwa tena kugombea uenyekiti na akalipiwa tena fedha za kuchukulia fomu na sasa Wazee wa Kigoma wamekuwa wa kwanza kujitokeza na kumchukulia fomu.

“Hivyo, nakubali kugombea tena kuiongoza CHADEMA kivingine, hakuna chama chochote kitakachokuwa na mtindo wa kufanya hivyo hasa katika chaguzi zake mbalimbali,”alitamba Mbowe.

Aliongeza kuwa kwa sasa atafanya kazi kubwa kivitendo zaidi na kutaka kila mwanachama kutoogopa na kutumika kwa kadri atakavyoweza ili kuhakikisha wanakijenga chama.

Mbowe alikabidhiwa fomu hiyo na Mzee Mapindo Saba kwa niaba ya wawakilishi wa Wazee wa mikoa ya Rukwa, Kigoma, Pwani, Dar es Salaam, Manyara, Iringa, Njombe, Zanzibari
Mwenyekiti huyo ambaye amekuwa akifanyiwa hujuma kutoka kwenye idara mbali mbali ikiwemo Idara  ya Usalama ya Taifa,ambao walimfanyia hujuma mwenyekiti huyo kwa Lengo la kudhohofisha Upinzani nchini.

No comments: