Sunday, August 17, 2014

KATIBA MPYA SASA NI MABISHANO,MBATIA NAYE AMJIBU WEREMA,SOMA HAPA

Na Karoli Vinsent

         SIKU moja kupita Baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kusema uwezekano wa kupata katiba mpya haupo, kutokana na Bunge  la Katiba  kukosekana Theluthi 2 ya wajumbe kutoka Zanzibar,kukosekana huko kunatokana na Wajumbe wanaounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kugoma kurejea kwenye Bunge hilo.
           
              Nao Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,Umeibuka na kumvaa Mwanasheria wa Serikali Jaji Fredrick Werema na kusema kama anajua katiba haipatikani kuna ulazima gani wa kutumia Mabilioni ya Watanzania kwenye Bunge hilo,  wakati Fedha hizo zingeenda kwenye masuala mengine ya Maendeleo ikiwemo kwenye kuboresha Daftari la Kudumu la wapiga kura.
              
         Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia wakati alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari,ambapo Mbatia alisema anamshangaa sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujua huwezekano wa kupata katiba mpya  haupo ,kwanini anashindwa kumshauri Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge hilo la Pesa kulekezea kwenye kwenye mambo mengine.

      
             “Nashangaa sana kwa huyo mwanasheria wa serikali anajua kabisa katiba haipatikana kwasababu ya Bunge hili kukosa Theluthi 2 ya wajumbe ambao wengi wao ndio sisi UKAWA ambao tumegoma kurejea kwenye bunge hilo kutokana na hujuma,ni bora tu Bunge hili livunjwe kwasababu katika haitopatikana kwa hali hii ilivyo,sasa yeye anasema bunge liendee,litaendelea vipi wakati anajua katiba haipatikani?”alihoji Mbatia.
         
            Mbatia ambaye naye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba alizidi kusema Mchakato wa katiba unaoendelea sasa katika Bunge Maalum la Katiba haujalenga kusimamia Maslahi mapana ya Watanzania kwa ujumla,bali umeporwa na kikundi cha watu wachache wnaotaka kutimiza malengo yao Binafsi hasa

kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
              
             Aidha,James Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais,alisema kwa hali ilivyo sasa ni Vema Bunge maalum la Katiba liharishwe mpaka pale muhafaka wa Kimataifa utakapopatikana kwa njia ya Maridhiano.
          
           Vilevile Chama cha NCCR mageuzi kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC iweke hadharani daftari la kudumu la wapiga kura liloboreshwa mwaka 2010 kwa kutumia mabilioni ya shiringi ya Watanzania,kwa kuwa chama hicho kimeshtushwa na taarifa za Tume kusema hakuna daftari wapiga kura.
          
                     Pia chama hicho kimezidi kushikilia msimamo wake wakutorejea kwenye Bunge hilo maalum la Katiba kwa madai mchakato huo wa katiba kuingiliwa na chama cha mapinduzi,na kusema Wajumbe waote wa Bunge maalum la Katiba wanaotokana na chama hicho,
           
             kutoshiriki katika vikao hivyo vinavyoendelea hadi madai ya msingi ya chama hicho pamoja washiriki wake ambao ni Vyama vya Chadema,CUF,DP na NLD yatakapopatiwa Ufumbuzi.    
          
            Kauli hiyo ya Mbatia inazidi inazidi kuwachanganya Watanzania kutokana na Viongozi wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuzidi kujichanganya kutokana hoja ya theluthi 2 ya wajumbe.
            
     Ambapo ikulu ya Kikwete katika tamko lake lilosainiwa na Kur
          ugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilisema Katiba Mpya itapatikana bila ya kuwepo UKAWA,kwani Theluthi 2 ya wajumbe inapatikana kwenye Bunge hilo.
    
            Na kuzidi kusema Umoja wa huo wa Ukawa ni Idadi ndogo sana,Kauli hiyo ya ukakasi ya Ikulu iliwai kutolewa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Samwel Sitta ,
       
            Baada ya Ikulu kutoa kauli hiyo,ndipo Jana Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema aliibuka na kupingana na Ikulu na kusema uwezekano wa kupata katiba mpya haupo, kutokana na Bunge hilo kukosa idadi ya Theluthi 2 ya wajumbe,na kusema endapo ikishindikana itabidi Bunge hilo lisimame na kutoa mwanya kwa Bunge la kawaida liifanyie marekebisho katiba iliyopo hususani kipengere cha tume ya uchaguzi na vingine,ili baada mchakato huu uendelee kama kawaida baada ya kumalizika uchaguzi Mkuu.

                 “Kuhusu Idadi ya kura za wajumbe wabunge maalum la katiba inatoa wasiwasi kwasababu kwenye Kamati zile theluthi 2 ya wajumbe inapatikana bila shida ila tatizo itakuja wakati wakupitisha Rasimu iliyojadiliwa na Bunge ndio itatupa shinda kwasababu lazima ipatikane theruthi ya 2 ya wajumbe wa Tanzania Bara na,”
      
             “ Zanzibar sasa ungiangalia hapa kwa hali ilivyo kama ikiendelea hivi bila ya kuwepo UKAWA itakuwa ni shida kupata Theluthi 2  ya awajumbe wa Zanzibar na hapa ndio watu wanasema tutakuwa tumetumia pesa nyingi sana za walipa kodi harafu hakuna katiba ndio maana nawaomba ukawa warejee”alisema Werema

No comments: