Thursday, August 21, 2014

LIVE--SHUHUDIA MAONYESHO YA BIDHAA ZA KICHINA YANAYOENDELEA DAR ES SALAAM,WAZIRI KIGODA AZINDUA RASMI MUDA HUU

Waziri wa viwanda na bisahara ABDALA KIGODA leo amezindiua rasmi maonyesho ya bidhaa za kichina nchini Tanzania maarufu kama BRANDS OF CHINA AFRICAN SHOWCASE 2014 maonyesho yanayoanza leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kumalizika tarehe 24 mwezi huu.

  Akizungumza katika uzinduzi huo asubuhi ya leo waziri kigoda amewataka wafanya biashara wa china hapa nchini Tanzania kuhakikisha wanaleta bidhaa zilizo na ubora unaostahili katika soko la tanzania ili kuepuka madhara yanayotokana na uwepo wa bidhaa feki katika soko.
Maonyesho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka nchini tanzania yakiwa na lengo la kuonyesha bidhaa bora ambazo zinapatikana china.

Waziri wa viwanda na biashara nchini MH ABDALA KIGODA akikata utepae rasmi kuashiria kufungua rasmi maonyesho hayo yanayofanyika jijini Dar es salaam



Picha zikionyesha watanzania mbalimbali wanaojitokeza katika maonyesho hayo hapa katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE 
Wafanya biashara mbalimbali kutoka nchini china wakonyesha baadhi ya bidha zao zinazopatikana katika maonyesho hayo 





Mwonekano katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE kwa sasa 


Waziri akitizama baadhi ya bidhaa zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo



No comments: