Thursday, August 21, 2014

MKE WA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MAMA DORCAS MEMBE AFUNGUA KITUO CHA KUSAMBAZIA MATREKTA CHA KARIATI MATRACTOR KILICHOPO KINONDONI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati (kulia), akimkaribisha mgeni rasmi Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe wakati akiwasili katika hafla ya kufungua kituo hicho kilichopo Kinondoni Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe (katikati), akisalimiana na Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo, ambapo wamekiwezesha kituo hicho kupata mikopo ya kununulia matrekta hao.
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati wakionesha tovuti ya kituo hicho baada ya kufungulia. Tovuti hiyo ya www.kariatimatractor.com itamsaidia mkulima yeyote aliopo nchini kupata fomu kwa ajili ya kununua matrekta hayo.
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe (katikati), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kusambaza Matrekta cha Kariati Matractor kilichopo Kinondoni Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Omary Kariatina Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB,
Victor Malewo, ambapo wamekiwezesha kituo hicho kupata mikopo ya
kununulia matrekta hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati (kulia), akimkaribisha mgeni rasmi Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe kusoma taarifa yake kwa wanahabari.
Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe akisoma taarifa yake kwa wanahabari.Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati (kulia), akizungumza na wanahabri na wageni waalikwa kwenye ufunguzi huo wa ofisi yake.
Watendaji katika ofisi hiyo wakimsubiri kumpokea mgeni rasmi. Kutoka kulia ni Samira Ambeyi, Endilt Manfred na Happy Msesa.
Wakulima kutoka Kijiji cha Kwadelo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wakiangalia mashine ya kupandia mahindi.
Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe akipeana mkono na Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo.
 
Dotto Mwaibale
 
MKE wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dorcas Membe amekitaka kituo cha kusambaza Matrekta kwa wakulima cha Kariati Matrekta kupunguza tena bei za bidhaa hizo ili kuwa kimbilio kwa wakulima.
 
Kauli hiyo ameitoa leo jijini  Dar es Salaa wakati akizindua kituo hicho ambapo alisema ingawa bei zao zipo chini wapunguze tena ili hata mkulima wa chini aweze kumudu kununua au kukopa trekta hiyo imuwezeshe kuondokana na umasikini.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo alisema anapongeza uanzishwaji wa kituo hicho kwani ni kazi inayowahusu wakulima ambao idadi yake ni takribani asilimia 80.
 
”Nakupongeza Mkurugenzi kwa jitihada za kuanzisha kituo hiki chenye lengo la kuwawezesha wakulima kupata matrekta na zana zake kwa fedha tasilimu au mkopo, mpango huo utawakomboa wakulima wengi kuondokana na jembe la mkono” alisema
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kariati Matrekta, Alhaji Omary Kariati alisema jambo ambalo wanalifanya ni kuunga mkono mpango wa Kilimo Kwanza wa serikali ya awamu ya nne  ya Rais Jakaya Kikwete kwa vitendo.
 
Aidha alisema kwa kuhakikisha wakulima wanapata dhana za kilimo hadi sasa tayari wamesambaza matrekta 80 ambapo wamekuwa wakikopesha bila ya dhamana.
 
”Nimeisikia mama akisema kuwa tupunguze bei na namuhakikishia hapa hapa kwamba tumepunguza tena bei   trekta la milioni 23 litanunuliwa kwa shilingi milioni 20”alisema
 
Mbali na hayo Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo amesema wanashirikiana vema na kituo hicho hivyo wakulima wategemee mambo mengi mazuri.

No comments: