Tuesday, September 30, 2014

ACT WAZIDI KUIANDAMA CHADEMA,VIONGOZI WENGINE WA CHADEMA LEO WATANGAZA KUHAMIA ACT

Na Karoli Vinsent

     CHAMA kipya cha Siasa cha Alliance for Change and Transparence-Tanzania ACT kiamezidi kukipasua chama cha Demokrsasia na Maendeleo CHADEMA kutokana wimbi la wanachama kukihama chama hicho na kujiunga na ACT.
          
          Wanachama hao kutoka CHADEMA wamejiunga na ACT leo na kupokelewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar Es Salaam wa chama hicho Hamisi Said Chambuso na kushuhudiwa na Waandishi wa Habari,ambapo Aliyekuwa mwenezi wa baraza la Wanawake la Chadema ,Jimbo la Kawe Batuli Abdalah naye alijiunga na ACT ,
        

          Batuli alisema sababu iliyomsukuma kujiunga na ACT ni kutokana kuchuka na siasa za ukabira zinazotawala chadema ambazo anadai zinasimamiwa na Viongozi wa Juu wa chama hicho akiwemo Freeman Mbowe,
        
         “Kiukweli mpaka nimeamua kujiunga na ACT ni kutokana na kuchoka na siasa za hovyo ambazo ni za udini na ukabila zinazofanywa na mwenyekiti Mbowe ambaye amekuwa akisisitiza hata katika vikao vya ndani kwamba kiongozi lazima atoke katika mkoa wa Kilimanjaro,na mimi nilipogundua Chadema hakina nia ya dhati ya kumuokoa mtanzania bali kinaendesha siasa za ukabila basi nimeamua kujiengua rasmi na kujiunga na chama cha ACT kutokana na kupendezesha na sera zake”alisema Mama Batuli
         
          Kwa upande wake aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema  kutoka mkoa wa Kigoma  Yassin Mohamedi naye alijiunga na Chama cha ACT Tanzania kwa madai ya kuchoshwa na Viongozi wa Juu wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kwa kuendesha siasa na ukabila badala ya kukijenga chama ili kiweze kumkomboa mtanzania  wa leo ambaye anakufa kwa umasikini,
         
        Wananchama wengine walijiunga na chama hicho ni Sylvester Kasongo aliyekuwa Afisa wa Chama cha Umma,na Eng Mohamedi Ngulanguma,
         
        Katika hatua nyingine chama Alliance for Chage and Transparence-Tanzania ACT kimepinga vikali Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba katiba na kusema Bunge hilo limekosa uhalali wa Kisiasa.
        
          Akisoma tamko la Chama  kwa Niaba ya viongozi wa juu wa chama ACT,Mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam Hamisi Said Chambuso,alisema chama hicho kinapinga vikali Rasimu iliyopendekezwa na Bunge kwani Bunge la Katiba limeshindwa kuleta usawa wa kisiasa badala yake limekuwa likitunga katiba ya chama kimoja.
  

No comments: