Wanafunzi nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vifaa vya
electronic mfano computer na simu za mkononi
kama njia moja wapo ya kujifunzia na kupata elimu badala ya kutumia kwa
nzia zisizofaa.
Wito huo leo umetolewa na mkurugenzi
wa kampuni ya mawasiliano ya tigo Tanzania DIEGO GUTIEREZ wakati akizungumza
katika hafla iliyoandaliwa na MICROSOFTna NOKIA kwa kushirikiana na wizara ya
mawasiliano sayansi na technologia ya uzinduzi wa (NOKIA MOBILE MATHEMATICS FOR
TANZANIA),kupata masomo ya sayans hususani somo la hesabu kwa njia ya simu za
mkononi na vifaa vingine.
Mkurugenzai huyo amesema kuwa kuna
dhana potofu iliyojengeka kuwa masomo ya sayansi hususani somo la hesabu ni
masomo magumu yasiyowezekana jambo ambalo amesema kuwa sio kweli kwani kwa
matumizi wa vifaa na huduma hiyo masomo hayo yatakuwa masomo pendwa kwa
wanafunzi wa Tanzania.
Huduma ya NOKIA MOBILE MATHEMATICS
FOR TANZANIA iliyozinduliwa leo ni huduma inayowawezesha wanafunzi kupata
masomo kwa njia za eleconic ambapo huduma hii ilianzia nchini Africa kisini
mwaka 2008 na Tanzania kuwa nchi ya pili kupata huduma hii, ambapo baada ya
utafiti kuonyesha kuwa wanafunzi wanapenda sana matumizi ya simu ikaonekana
huduma hii itawasaidia wanafunzi katika masomo hayo.
Katika hatua nyingine kampuni yaTIGO
Tanzania imeahidi kutoa FREE DATA kwa wanafunzi wote watakao kuwa wanatumia
huduma hii ya NOKIA MOBILE MATHEMATICS FOR TANZANIA.
No comments:
Post a Comment