BREAKING NEWZZ-CHADEMA WATANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA BARAZA LA WAZEE LA CHAMA HICHO,MZANZIBAR AIBUKA KIDEDEA UENYEKITI

Mkurugenzi wa kampeni wa CHADEMA SINGO BENSON  akitangaza matokeo ya uchaguzi huo muda huu jijini Dar es salaam
 Chama  cha Democrasia na maendeleo chadema muda huu kimetangaza matokeo ya uchaguzi wake wa kwanza wa chaguzi zake za ndani ya chama ambapo kwa safari hii ni uchaguzi wa baraza la wazee la chama hicho uchaguzi uliofanyika juzi tarehe  6 jijini dare s salaam na kumalizika usiku.
Akizungumza na wanahabarai muda huu makao makuu ya chama hichi konondoni jijini dare s salaam mkurugenzi wa kampeni wa chama hicho SINGO BENSON KIGAIRA amesema kuwa uchaguzi huo ulimalizika kwa amani na baraza hilo kupata viongozi wake wapya ambao watadumi katika nafasi hizo kwa muda wa miaka mitano kuanzia sasa.
Mwenyekiti mpya wa baraza la wazee la CHADEMA mzee HASHIM JUMA ISSA akitambulishwa mbele ya wanahabari muda huu baada ya kuibuka mshindi katia uchaguzi huo
 Akitaja majina ya wagombea nafasi ya mwenyekiti wa taifa wa baraza hilo la wazee ameshinda mzee HASHIM JUMA ISSA kutoka Zanzibar ambaye ametangazwa rasmi kuwa mwenyekiti mpya wa baraza hilo la wazee la CHADEMA taifa.
Nafasi ya makamu mwenyekiti wa baraza hilo la wazee kwa upande wa bara imechukiliwa na mh SUZAN LYIMO ambaye sasa ametengazwa rasmi kuchukua nafasi hiyo,huku nafasi ya makamu mweyekiti wa baraza hilo kutoka zanzibari ikichukuliwa na mzee OMAR MASOUD OMAR.
MH SUZAN LYIMO ambaye kwa sasa ni makamu mwenyekiti  bara akitambulishwa pia

 Katika nafasi ya katibu mkuu wa baraza hilo la wazee la chama hicho aliyeshinda ni mzee RODRICK EMMANUEL LUTEMBEKA ,huku nafasi ya mwekahazina wa baraza hilo ikichukuliwa na ERASTO SINGIRA GWOTA .
Aidha katika nafasi ya ujumbe wa baraza kuu taifa KUTOKA BARA  walioshinda ni ALFRED NTUPWA,FLORENCE KASILIMA,HUGO KIMARYO, pamoja na VICTOR KIMESERA.huku nafasi ya ujumbe wa baraza kuu kutoka Zanzibar ikichukuliwa na HASHIM JUMA ISSA pekee baada ya wajumbe wengine wawili kujitoa kabla ya uchaguzi huo.
Mwenyekiti mpya wa baraza la wazee la CHADEMA mzee HASHIM JUMA ISSA akitoa neno la shukrani kwa kuchaguliwa ambapo pamoja na mambo yote amesisitiza kuwa nia yake ya kiugombea katika nafasi hiyo tena akitokea upande wa pili wa Tanzania ni kuhakikisha anaikomboa ZANZIBAR na kuipata ZANZIBAR huku tofauti na sasa ambapo amesema kuwa haipo huru.

Nafasi nyingine iliyokuwa inahitajika ni nafasi ya wajumbe wa mkutano mkuu kutoka bara ambapo waliochaguliwa ni CHARLES KIKOMINGO,MARY NAKOE,MARRY JOACHIM,SYLIVESTER SHIRIMA,TIMOTH KIRWAY,pamoja na WILLIAM MWANGWA huku kutoka Zanzibar wakiwa  ni HASSAN KHERI,KHATIBU ALLY KHATIBU,HAJI KALI HAJI,pamoja na RABIA,OMAR

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.