.

breaking newzz--SOMA NA SIKILIZA SENTENS TATU KALI ALIZOTOA WAZIRI MWAKEMBE JUU YA AJALI YA JANA

  1. Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenz
    ake na kusema mimi lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe
  2. Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’
  3. Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.