Monday, September 29, 2014

HABARI NZURI TOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA LEO

Na Karoli Vinsent

        MAMLAKA ya Hali hewa nchini(TMA) imezindua Jarida Maalum  lenye kutoa taarifa za matukio ya hali ya hewa kwa mwaka husika ambalo litakuwa likiwapa nafasi wananchi kujua halli ya hewa ya mwaka mzima,

           Uzinduzi wa jarida hilo umefanyika Leo Jijini Dar Es Salam na kushuhudiwa na Waandishi wa Habari pamoja na Wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA),ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt.Agnes Kijaz alisema Jarida hilo linalengo la ekulezea umma hali ya hewa ilivyokuwa katika kipindi cha mwaka husika kwa ufipi,
     

            Vilevile Dkt Kijazi alizidi kusema Jarida hilo litatoa maelezo mafupi ya kitaalum ya sababu za kutokea kwa mafuriko nchini ,hivyo Jamii itaweza kujua zaidi ya nini sababu za Mafuriko makubwa yanaoyotokea nchini,
        
        Aidha Dkt Kijazi aliwataka watanzania kujitokeza kulisoma jarida hilo hili waweze kupata taarifa mbalimbali zinahusu Mamlaka hiyo,ambapo Jarida hili litapatikana kwenye Maktaba ya Taifa,kwenye mtandao wa Mamlaka hiyo,pamoja na ofisi zao zilitambaa nchini nzima.
     
       Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya hewa James Ngeleja,aliipongeza TMA kwa kazi kubwa inayofanywa na kuwataka watanzania kulisoma jarida hilo kwa umakini ili kuweza kupta ufahamu zaidi kuhusu hali ya hewa nchinii,
        
       Jarida hilo litaanza kuyaangazia matukio ya hali ya hewa kwaanzia mwaka 2011. 

No comments: