HIVI NDIVYO SIMBA YA OKWI NA KIONGERA ILIVYONYANYASWA TAIFA NA URA

Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi kushoto akiwatoka mabeki wa URA ya Uganda jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. URA ilishinda 1-0.

SIMBA SC imepoteza mechi ya kwanza chini ya kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na URA ya Uganda katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bao hilo pekee la timu hiyo ya Mamlaka ya Mapato Uganda lilifungwa na Frank Kalanda dakika ya 42, akimalizia krosi ya Elkanda Nkungwa aliyefanikiwa kumtoka Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. 

Pamoja na kufungwa, Simba SC ilicheza vizuri na jioni ya leo bahati haikuwa ya kwao, kwani walipoteza nafasi zisizopungua tano za kufunga mabao.URA pamoja na kuwasili Saa 6:00 usiku wa jana, lakini haikuonyesha uchovu badala yake ‘iliipelekesha’ Simba SC na kama si jitihada za kipa Ivo Mapunda kuokoa michomo mingi ya hatari, wangeweza kupata mabao zaidi.Baada ya mchezo wa leo, SImba SC inaelekea Mtwara m
apema asubuhi ya kesho kuungana na wachezaji wengine waliotangulia wakiongozwa na Amisi Tambwe kwa ajili ya mechi na Ndanda, ya kirafiki pia.

Mchezo na Ndanda ndiyo utakuwa wa mwisho kwa Simba wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wiki ijayo, Wekundu hao wa Msimbazi wakifungua dimba na Coastal Union ya Tanga Septemba 22, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   

Awali, Simba SC chini ya Phiri aliyerithi mikoba ya Mcroatia Zdravko Logarusic mwezi uliopita, ilishinda 2-1 dhidi ya Kilimani FC, 2-0 dhidi ya Mafunzo na 5-0 dhidi ya KMKM zote Uwanja wa Aamaa, Zanzibar na 3-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa.

Simba SC; Ivo Mapunda, Miraj Adam, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Pierre Kwizera, Ramashani Singano ‘Messi’, Amri Kiemba/Paul kiongera dk49, Emmanuel Okwi, Shaaban Kisiga na Haroun Chanongo/Uhuru Suleiman dk62.

URA; Bwete Brian, Massa Simeon, Munaabu Alan, Samuel Ssenkoom/Ronald Sekubomba dk64, Jonathan Mugabi, Oscar Agaba, Feni Ali, James Kasibante/Ngama Emmanuel dk57, Said Kyeyune, Elkanda Nkugwa/Augustino Nsumba dk64na Frank Kahan

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.