Thursday, September 11, 2014

KAMA ULIKUA HUJUI NI KWAMBA PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA,SOMA TAARIFA YA OFISI YA TAKWIMU LEO


Na Karoli Vinsent

     HUKU kukiwa hali ya Umasikini kwa Watanzania ikizidi kuongezeka  kila kukicha,Lakini hali ya  Pato la Taifa linazidi kuongezeka   hadi kufikia asilimia 7.4  tofautisha na mwaka jana 2013 pato la Taifa lilikuwa kwa 7.1.  
         
        Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Morice Oyuke 
(PICHANI) wakati  akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  wakati akitoa taarifa ya pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka kuanzia Januari na Machi 2014,ambapo amesema Pato hilo la Taifa limeongeza kwa kasi nzuri tofautisha na mwaka jana.
            
            “Ukuaji wa pato la Taifa kwa bei ya soko uliongezeka kwa kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2014 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 7.1 katika kipindi cha mwaka cha mwaka 2013,na kielezo namba 1 jumla ya thamani ya pato la taifa katika kipindi husika ilikuwa shilingi 4,862,689 milioni mwaka 2014 ikilinganishwa na shilingi 4,526,148 milioni mwaka 2013”alisema Oyuke.
           



       Oyuke alizidi kusema ukuaji huo wa pato la Taifa umetokana na Mchanganuo wa ukuaji wa Shunghuli za Kiuchumi kwenye pato la Taifa kwa Robo ya mwaka 2014 katika sehemu tofauti,
             
       Aliyataja sehemu hizo ni kilimo na uvuvi,ambapo katika sehemu hii Shughuli za Uchumi za Kilimo zilifikia kasi ya ukuaji ya Asilimia 1.6 katika kipindi cha Robo mwaka ya Kwanza 2014 ikiwa ni sawa na Iliyofikiwa katika kipindi kama hicho 2013.
             
         Pia katika sehemu nyingine ni Viwanda ma Ujenzi Shughuli za uchimbaji madini,mawe na kokoto ziliongezeka na kufikia kasi asilimia 8.7 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka  2014 ikilinganishwa na  kasi ya ukuaji wa asilimia hasi 1.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2013,
           
        Napo  Sehemu nyingine ni upande  Shughuli za Uchumi za Utoaji Huduma ambapo Shughuli za Biashara za Jumla na Rejareja,ukarabati wa Magari na pikipiki na Vifaa vyengine vya majumbani vilifikia asilimia 8.0 katika kipindi cha robo mwaka na imekuwa tofauti mwaka jana,
   
      Aidha Mkurugenzi Huyo wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Morice Oyuke alisema Ofisi hiyo ya Takwimu itasambaza  takwimu za pato la Taifa  kwa robo mwaka pili (Aprili-juni 2014) tarehe 30 semptemba 2014 kama ilivyo kwenye shajala ya machambisho kwa lengo la kuweka ukweli


No comments: