Thursday, September 11, 2014

HABARI KUBWA LEO--MBOWE ALIPUKA,ASEMA WANAWAKE WAZEMBE HAWANA NAFASI CHADEMA,SASA UKAWA KUFUNGA KAZI MWISHO WA WIKI HII,SOMA YOTE HAPA


Mwenyakiti wa CHADEMA taifa MH  FREMAN MBOWE akiwasili ukumbi wa mliman city kwa ajili ya kuzungumza na wamama wa chama hicho mapema leo
 Mwenyekiti wa chama cha demcrasia na maendeleo (chadema) taifa mh FREMAN MBOWE amesema kamwe wanawake wa chama hicho wasitarajie kupewa nafasi za upendeleo katika uongozi wa chama hicho kwani chama chake hakipo kwa ajili ya kugawa zawadi ya vyeo na badala yake wajitume kuhakikisha wanakuwa na uwezo unaotakiwa katika kuongoza chama hicho.
Kauli hiyo ameitoa muda huu jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanawake wa chama hicho nchi nzima wakati akifungua mkutano wa baraza la wanawake la chadema BAWACHA mkutano ambao utaitimishwa kwa kupatikana viongozi wapya wa chama hicho.
MH MBIOWE ambapo muada mwingi ameonekana kuwasihi wanawake kuacha majungu ndani kwa ndani na badala yake wafanye kazi ya kujenga chama hicho kwa lengo la kuchukua dola mwakani
Mh MBOWE amesema kuwa hakuna kubebana  katika maswala muhimu kama uongozi kwani chadema ni chama makini na ni lazima kuhakikishe kuwa kinakuwa na viongozi makini na wenye uwezo wa kuleta mabadiliko ndani ya nchi hivyo hakitakuwa na msamaha wowote kwa mwanamke ambaye atadhani kuwa anastahili kupewa uongozi hata kama hana sifa za kuwa kiongozi.

“ndugu zangu wanawake naomba muelewe jambo moja,pamoja na kuwa tunatakiwa kuhakikisha kuwa wanawake wanawezeshwa ili wawe na haki sawa na wanaume lakini hatuwezi kutenda dhambi ya kumpa mtu cheo hata kama hana sifa eti kwa sababu ni mwanamke,hatutoi zawadi ya vyeo ndani ya chama chetu,tunahitaji wanawake majasiri,wenye moyo wa kuwakomboa watanzania,hivyo kama umegombea nafasi yoyote katika chama hichi ukidhani kuwa tutakubeba kwa kuwa wewe ni mwanamke mimi nasema hatuko tayari”amesma mbowe.
 Akizungumzia mchakato wa katiba mpya na ulipofikia mh MBOWE amesema kuwa wao kama UKAWA sasa wamechoka na michezo wa kitoto ambao amesema unachezwa na baadhi ya viongozi wa ccm juu ya mchakato huu hivyo sasa wameamua kufanya jambo tofauti ambapo amesema kuwa jumapili ijayo umoja wao wameamua kukutana na watanzania wote kwa wakati mmoja na kuwaeleza ukweli wote wa kwanini mchakato huo umekwama ambapo hakutaja njia ambayo wataitimia kukutana na watanzania wote kwa wakati mmoja.
Mbunge wa ubunge MH JOHN MNYIKA naye alikuwepo katika mkutano huo

Wanawake kutoka kila kona ta TANZANIA wakicheza kwa furaha muziki kabla ua kuanza kwa shughuli hiyo rasmi

Mama GETRUDE MONGERA alikuwepo kuwapa maneno mazuri wanawake wa tanzania ambapo amesema kuwa lazima wanawake wa TANZANIA wawe na umoja bila kuweka itikadi zao za vyama kwa ajili ya maendeleo ya mwamake wa kitanzania

Hapa lilitumika neno moja tu pipoooooooooooooooooo------
  “naomba nisema machache juu ya mchakato wa katiba,unajua kuna mchezo mchafu sana tunachezewa ila mi nasema ni wakitoto sana,sisi kama ukawa tumeamua kuwaeleza watanzania wote mwenendo wa mchakato mzima siku ya jumapili na naomba wanawake mttunge mkono”
Aidha amesema kuwa katiba mpya lazima ipatikane hata miaka mia ijayo itapatikana tu ila cha msingi ni kupata katiba itakayowasaidia watanzania wote na sio kuwasaidia wachache kama ilivyo sasa.




Baraza la wanawake la chadema BAVICHA linaingia katika mchakato wake wa kuwapata viongozi  wapya ikiwa ni baada ya hapo jana baraza la vijana BAVICHA kufanya uchaguzi wao ambapo  bw PASTROBAS PASCAL aliibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti akichukua mikoba ya JOHN HECHE aliyemaliza muda wake.
Mamia ya wanawake wa chama hicho wakiwa wanasikiliza kwa makini katika mkutano huo ambao unaendele hapa mlimani city jijini Dar es salaam


No comments: