Friday, September 26, 2014

KUHUSU MAMBO MAKUBWA WALIYOZUNGUMZA UKAWA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM USIKOSE HAPA

Mwanasheria wa chama cha democrasia na maendeleo chadema TUNDU LISSU (kushoto) pembeni ni mwenyekiti wa chama hicho mh FREMAN MBOWE pamoja na viongozi wa ukawa walivyokutana na wanahabari leo njijini dar es salaam
Na Karoli Vinsent

LICHA ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta kujinadi kwamba Theluthi 2 ya wajumbe inapatikana wakati wa upigaji kura kuipitisha rasimu  iliyopendekezwa na Bunge hilo, kwa madai wajumbe Bungeni hapo wasiokuwepo watatumia hata njia ya Fax,simu pamoja na “Internet” mtandao  kupiga kura,
           
Nao Viongozi Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umemjia juu Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo chake cha Kumwacha mwenyekiti wa Bunge hilo Samwel Sitta kwa kuendelea kufanya hujuma kwa watanzania kwenye mchakato wa katiba,
         
  Kwani Duniani kote hakuna kura yeyote inayopigwa kwa njia ya simu wala Internet na anavyofanya hivyo samweli sitta ni kutaka kufanya mambo pasipo kisheria,
           
Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Viongozi wa  vyama vikuu vya upinzani nchini wanaounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuyakimbia matatizo nchi na kwenda nje ya nchi na kushindwa kuliokoa taifa katika hujuma  anayofanya Samwel sitta.
        
“Rais Kikwete amekuwa mtu wa kwenda Marekani kila wakati yanapotokea Matatizo,na leo anamwacha Samwel Sitta anafanya mambo ya ajabu, ambayo duniani hayajawai kutokea kura kwa njia ya simu,harafu Rais Kikwete anashindwa kukemea uragai huu,hivi huyo ni kiongozi gani”Alihoji Profesa Lipumba
           


Profesa Lipumba ambaye ni Gwiji la masuala Uchumi kimataifa alizidi kuzungumza kwa Uchungu ambapo alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kuonyesha ugeugeu kwa watanzania kwani wakati wa Mkutano kati yake na Vyama vya kisiasa nchini vilivyo chini ya Kituo cha Demokrasia nchini ( TCD).
          Katika mkutano huo Rais Kikwete alikubali wazi kwamba bunge Maalum la sasa aliwezi kuleta katiba cha kushangaza leo  ameshindwa hata kuingilia kati utoto unaofanywa na Samwel Sitta kwa Watanzania.

        Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe naye pia alimshangaa Rais Jakaya kikwete kushindwa kuongoza nchi na kukimbilia Marekani na kumwachia Samweli sitta ndio kiongozi wa nchi na kufanya mambo ya hovyo katika Bunge la Katiba.
        “Rais kikwete amekosa hata utashi kuliokoa Bunge hili, yeye analikimbia Tatizo anakwenda Marekani,yaani leo Sitta anakuwa na Sauti kuliko Kikwete,jamani watanzania wenzangu nchi hii haina kiongozi huyo, ndio kiongozi kweli leo anashindwa hata kuwaonea huruma watanzania wanavyolia na Umasikini,leo mapesa yanapotea hivi”alisema Mbowe,

  Aidha Mbowe alizidi kutoa masikitiko yake kwa Rais kikwete kwa kuonyesha wazi kwamba ni watu wakubadilika badilika na kushindwa kusimama kwenye msimamo sahihi na wenye tija kwa manufaa kwa taifa,kutoka na kushindwa kusimamia maazimio aliyoyatoa Kwenye mkutano kati yake na Vyama vya Kisiasa
        
 “Jamani nataka mumfahamu Rasi Kikwete alivyo,wakati wa kutano baina yangu na yeye au Viongozi wa Vyama vya Kisiasa ambao waliokuwepo hadi viongozi CCM Kinana na Mangura,katika Mkutano huo anakubali wazi katiba haiwezi kupatikana na Bunge hili na tena tunakubaliana wote mchakato uendelee baada ya uchaguzi mkuu,sasa inakuwaje leo wakina sitta wamekuwa wanaipinga kauli yake hivi Rais unakuwa Kimya kiasi hichi na kukimbilia Marekani,kwa mfumo nawaomba watanzania wajipime”alisema Mbowe
       
 Kuhusu hukumu ya Kesi iliyofungiliwa na Mwandishi wa Habari Mwandamizi Saed Kubenea Katika kesi hiyo, Kubenea aliyekuwa akiwakilishwa na mawakili, Peter Kibatara na Mabere Marando, anaitaka Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya mwaka 2011 na Mahakama hiyo kutoa hukumu Maoni ya wananchi yaheshimiwe na kusema hayo mengine mahakama hayawezi kuyatolea ufafanuzi kwa madai ni yakisiasa,
      
      Mwanasheria Mkuu wa Umoja wa Kutetea katiba ya Wananchi Tundu Lissu aliishangaa Mahakamu kuu kugundua Bunge la Maalum la Katiba kwamba limefanya Makosa kuzika maoni ya yaliyotolewa na Jaji Warioba na kushindwa kuchukua hatua badala yake Mahakama hiyo imeishia tu kusema suala hilo ni la kisiasa kwani kufanya hivyo kuzidisha mashaka kwa mahakama kuu,
     Kuhusu maandamano na mikutano ya Ukawa kukataliwa na Jeshi la Polisi nchini.
     
   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe alisikitika kwa Jeshi la Polisi kuwanyima haki ya Msingi Kikatiba ya Kufanya Maandamoni kwani yeye anashangaa Jeshi hilo kukiruhusu chama cha Mapinduzi CCM kiendelee kufanya Mikutano yao huku kikiwakataza Chadema,CUF,wasifanye mikutano.

 
   Kiongozi wa Afrika ya Kusini Mzee Nerson Mandela alisema Serikali yeyeto inayotumia Mabavu kuwanyima haki wananchi basi wananchi watachoka watatafuta njai nyingine kudai haki,kiukweli leo Chadema tukitaka hata kufanya mikutano majimboni kwetu tunakataliwa na jeshi la polisi,lakini Kinana anaruhisiwa kuendelea kujinadi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa sisi tunakatazwa ,mimi mwenyewe nilitaka kwenda Jimboni kwangu nimezuliwa na polisi jamani haki za msingi tunanyimwaalisema Mbowe.





No comments: