Thursday, September 25, 2014

WANAFUNZI WA TAMBAZA WAPEWA SOMO NA TAASISI YA WAANDISI NCHINI

Na Karoli Vinsent

       KATIKA kuonyesha imedhamiria  kuhakikisha wanapatikana Waandisi bora nchini,Taasisi  ya Waandisi Nchini(Istitution of Engineer Tanzania IET) imewataka wanafunzi  kuacha kusomea masomo ya sanaa peke yake badala yake wajikite zaidi kwenye masomo ya sayansi ili kulisaidia Taifa liweze kupata waandisi wenye sifa,

            
      Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Rais wa Taasisi ya waandisi Tanzania (IET) Injinia Dokta Malima Bundala wakati alipokuwa anatoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu Waandisi katika Shule ya Sekondari Tambaza ambapo alisema ni wakati umefika wanafunzi watanzania wakabadilisha mawazo na kuanza kuyapenda masomo ya Sayansi na kuliokoa taifa , kutokana na kukosa kwake wataalumu wamasuala ya sayansi.
            
    “Taasisi ya waandisi nchini imeamua kufanya shughuli za maendeleo na leo tumeanzia katika shule hii ya tambaza kwa lengo la kuja shuleni hapa ni kutoa elimu kwa wanafunzi kuyapenda masomo ya sayansi na kuliokoa taifa lilipo sasa kwa kukosa wataalamu mbalimbali wa masuala ya sayansi ,kwani mambo haya ya uandisi ni mazuri katika kulisogeza taifa lipige hatua”alisema Dokta Bundala,
     
            Dokta   Bundala alizidi kusema wanafunzi wengi nchini wamekuwa waoga katika kusomea mambo ya uandisi kwa kisingizio cha kukosa ajira lakini jibu ni hapana kwani mambo ya Uandisi yanatoa uwanda mpana kwa mwanafunzi anapomaliza shahada yake na kuweza kujiajiri,
         
         Kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule hiyo ya Sekondali ya Tambaza Ratifa Juma aliipongeza taasisi ya Waandisi nchini kwa elimu waliyoitoa kwani elimu hiyo imewafungua macho na kuanza kuyapenda mambo ya Uandisi,
       
          Naye mwanafunzi Mwengine wa shule hiyo Bahati Wiliam John naye akisita kuipongeza Taasisi hiyo na kusema imewafanya wafahamu vitu vingi ambavyo walikuwa hawavijui kuhusu mambo ya uandisi na akaitaka Taasisi hiyo kuwa na utamaduni wakupita kila mara katika shuleni hapo na shule zengine ili iwasaidie wanafunzi wengine wenye mawazo hasi kuhusu mambo ya waandisi.
              
      Huu ni Mwendelezo wa Shughuli za Kijamii zinazofanywa na Taasisi hiyo kwani ilianza kufanya hivyo tangu semptemba 21 mwaka huu na hadi tarehe 26 kwa kupita sehemu mbalimbali ikiwemo shule pamoja sehemu zengine kwa lengo la kutoa elimu kwa Watanzania.

No comments: