.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO KATI YA VYOMBO VYA HABARI NA VYOMBO VYA ULINZI, USALAMA NA SHERIA, JIJINI DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano wa Mashauriano kati ya Vyombo vya Habari na Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2014. Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania 


Rais wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Jaji Thomas Mihayo, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo,  uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Kajubi Mukajanga, akizungumza kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo,  uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Washiriki, waandishi wa habari na Wahariri wa habari kutoka Vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kufungua rasmi mkutano huo leo.  Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Kajubi  Mukajanga, wakati akiondoka mara baada ya kufungua mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Asah Mwambene

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati akiondoka katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, baada ya kufungua mkutano huo

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.