Tuesday, September 30, 2014

MAMBO SITA AMBAYO BARAZA LA WAZEE LA CHADEMA LIMEITAKA CCM KUWATIMIZIA WAZEE WA TANZANIA

Mwenyekiti wa Baraza la wazee CHADEMA mzee HASHIM JUMA ISSA (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam kushoto ni makamu wake SUZAN LYIMO na RODRIC LUTEMBEKA katibu wa baraza hilo
Ikiwa kesho tarehe 1,mwezi wa kumi dunia inaadhimisha siku ya wazee  duniani baraza la wazee la chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA limeibuka na mambo sita ambayo wameitaka serikali ya CCM kuwajibu wazee kwani ndio kero za wazee kwa muda mrefu.

Akizungumza na waandiishi wa habari makao makuu ya chama hicho muda huu mwenyekiti wa baraza hilo mzee HASHIMJUMA ISSA ametaja mambo hayo kuwa ni


1-kwanini rasimu ya katiba mpya inayolazimishwa na ccm imeshindwa kuzingatia haki za wazee ya universal pension baada ya wao kutumia umri wao kulitumikia taifa katika secta rasmi na zisizo rasmi (wakulima,wafanyakazi,wafugaji,nk.

2-kutolipwa pension kwa wakati baada ya kustaafu(kwa wafanyakazi walioko kwenye secta rasmi)

3-kukosa makazi (vituo) vyenye hadhi au kutelekezwa kabisa.

4-kukosa jukwaa la kutoa michango ya mawazo yanayogusa maisha yao na jamii kwa ujumla.

5-kudanganywa kuhusu matibabu bure,wakati ukweli ni kwamba hakuna huduma hiyo na hata ikipatikana ni kwa mashartihuku ikiwa haina ubora kama zilivyohuduma nyingine za kijamii chini ya uongozi wa serikali ya ccm.

6-kutoshirikishwa katika mipango ya kiuchumi kuinua maisha yao.

Aidha mwenyekiti huyo amewataka wazee wa Tanzania kuliombea taifa lao kwani lipo katika kipindi kigumu cha ombwe la uongozi wa CCM na kuwataka kutoka hadharani kukemea mambo ya ubadhilifu yanayoendelea nchini.

Katika hatua nyingine wazee wa chadema kesho watakwenda kuwatembelea wazee wanaoishi katika makazi ya wazee wa nunge-kigamboni ili kijumuika nao katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.

No comments: