.

MWIGULU NCHEMBA ATULIZA MGOMO WA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO,SOMA KAULI YAKE HAPA

Na Karoli Vinsent

   NAIBU Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba  ameitaka Mamlaka ya mapato nchini (TRA)kusitisha mara moja mpango wake wa kuyafungia Maduka ya wafanya biashara ndogondogo nchini,badala yake ameitaka Mamlaka hiyo itatue changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.
        
          Hayo yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyikiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Johson Minja wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliotishwa mahususi kwa ajili ya kuzungumzia Mkutano mkuu wa Dharura uliitishwa na Wafanyabiashara nchi nzima, uliofanyika Dodoma Mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba aliiwakilisha Serikili kwenye mkutano huo,
     
       Ndipo katika Mkutano huo wafanyabiashra walimuelezea Changamoto Mbalimbali zinazowakabili kuhusu mfumo mpya wa Mashine ukusanyaji kodi ya Kitroniki EFD,

      Baada ya kuwasikiliza wafanyabiashara hao,Mwigulu nchemba aliwaamuru mara moja Mamlaka ya Mapata nchini TRA kuacha kuyafungia maduka yasiyokuwa na Mashine za EFD .

         “katika mkutano na Mwigulu Nchemba kwa kuwa ndio mtu mwenye mamlaka ya juu kimaamuzi na kumweleza changamoto zinazotukabili wafanya biashara na akutuelewa ndipo akafikia maamuzi ya   kuwaomba TRA waache kuyafungia maduka na kutatua changamoto zinazowakabili wafanya biashara  kuhusu mfumo huu wa ukusanyaji kodi wa Mashine za EFD,”alisema Minja.


        Minja alizidi kusema Naibu waziri huyo aliendelea kutoa maamuzi  mengine ikiwemo Kubadilisha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la thamini,VAT,kushughulikia ombi la kuwa na kipindi cha kufanya biashara bila kulipa kodi kwa wafanyara wapya pamoja kwenda kupitia makabrasha aliyokadhiwa yenye hadibu za rejea za vikao vya kamati na baadae atawaita kutoa maamuzi,
About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.