Monday, September 22, 2014

PICHA 20--HILI NDILO TUKIO KUBWA LEO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Kamishna wa kanda maalum ya dar es salaam SUKEMAN KOVA akiwasili katika viwanja vya polisi osterbay tayari kabisa kuhudhuria sherehe hizo za ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
 Wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa kanda ya Dar es salaam imezinduliwa leo muda huu na mkuu wa wilaya ya kinondoni mh  Jordan Rugimbana katika sherehe zilizofanyika katika makao makuu ya pilisi wilaya ya kinondoni ostabay jiji,na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo kamishna wakanda maalum ya dar es salaam SULEMAN KOVA na makamanda wengine wengi pamoja na wananchi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam.

Akizungumza wakati akisoma risala iliyokuwa isomwe na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa dar es salaam mh SAID MECK SADIC mkuu wa wilaya ya kinondoni mh Jordan Rugimbana  amewatahadharisha madereva na watumiaji wa barabara kuwa makini pindi wawapo barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikijitokeza kutokana na uzemba wa madereva na watuamiaji nwa barabara kwa ujumla.
wiki ya nende kwa usalama baranbarani kitaifa itafanyika mkoani arusha na leo ndio uzinduzi umefanyika huko.
HAPA NI BAADHI YA PICHA ZA SHEREHE HIYO YA UFUNGUZI ILIYOMALIZIKA MUDA MFUPI ULIOPITA.picha zote na EXAUD MTEI

Kamishna kova akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya kinondoni wakati wa shughuli hiyo.
Wanafunzi ni sehemu ya wageni waliofika hapa ili kupata elimu ya usalama barabarani inayotolewa hapa
Kikundi cha sanaa ambacho kilikuwa kikitoa burudani wakati wa uufunguzi huo

Maandamano kuingia uwanjani hapo yalifanyika kutoa jumbe mbalimbali kuhusu wiki hii




Kamishna wa kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA akitoa elimu ya usalama barabarani mbele ya watu waliohudhuria katika sherehe hizo fupi leo jijini Dar es salaam
Mkuu wa wilaya ya kinondoni mh Jordan Rugimbana akisoma hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye alitoa hudhuru mkuu wa mkoa wa Dar es salaam SAID MECK SADIC 
Picha ya pamoja
Mkuu wa mkoa wa kinondoni akikata utepe kuashiria kuwa wiki ya nenda kwa usalama barabarani imezinduliwa rasmi leo katika kanda ya Dar es salaam ambapo kitaifa inafanyika arusha
Mgeni rasmi akipata maelekezo mbalimbali kutoka katika mabanda yanayotoa elimu ya usalama barabarani katika viwanja hivyo



No comments: