Monday, September 22, 2014

SERIKALI YAWATEMA WAANDISHI WALIOPIGWA,YASEMA HAKUNA MWANDISHI ALIYEPIGWA WOTE NI WANACHAMA WA CHADEMA

Na Karoli Vinsent

        HUKU wadau mbalimbali wa Habari wakiwa wanalaani Vikali kitendo cha Jeshi la polisi kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini,tukio hilo lilitokea Mwishoni mwa wiki iliyopita Makao makuu ya Jeshi la polisi nchini ambapo mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alipofikishwa  polisi,
          
           Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu ya kupigwa kwa mwandishi,bali imesema inafahamu tu wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndio waliokwenda makao makuu ya Jeshi la Polisi,na hawafamu kwamba kunawanahabari waliopigwa,

            
         Kauli hiyo ya Kushangaza imetolewa leo jijini Dar Es  Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,Asah Mwambene wakati alipokuwa anatembelea Mradi wa Maendeleo wa Shirika la tanesco uliopo Mbagala Jijini Dar Es Salaam,licha ya kuzungumia masuala mbalimbali kuhusu Tanesco kufikisha Miaka 50 ya kutuo huduma,
          
          Ndipo Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi alipomuuliza Mkurugenzi huyo kwamba yeye kiongozi wa Waandishi wa habari anazungumziaje kitendo cha Jeshi la Polisi kuwapiga waandishi wa habari walipokuwa kazini wiki iliyopita.
         
         Ambapo Mwambeni ambaye  vilevile pia ni Msemaji wa Serikali alisema hana taarifa za kupigwa waandishi wa habari bali anacho fahamu yeye ni wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema walikwenda polisi.
    
           “Serikali haina taarifa za kupigwa kwa waandishi Serikali inachojua ni wanachama wa chama cha Chadema ndio walikwenda kwenye jeshi la polisi na sio waandishi wa habari,na tunachojua sio waandishi wa habari waliopigwa,nakuomba tuzungumeze vitu vingine ”Alijibu Mwambene.
         
              Baada ya Mwambene kuzungumza kauli hiyo,alitoka pembeni akawa anaongea na Mwandishi wa Gazeti la Habari leo ambaye naye ni Miongoni mwa Waandishi wa Habari waliopigwa na jeshi la polisi katika Tukio hilo huku akirekodiwa na mwandishi wa Mtando huu bila ya yeye kujua kwamba mwandishi wa Mtandao huu anayafuatilia mazungumo hayo alisikika akisema

        “Ni mwandishi mmoja tu anayelalimika  sana kwenye Vyombo vya Habari,ni Yule Josephat isango wa gazeti la Tanzania daima Yule tunajua kabisa ni mwanachama wa chadema kabisa maana aliwai kugombania Ubunge kupitia chama hicho na tunachojua sisi na hata polisi waliokuwa wakimpiga wanamjua Yule ni chadema ndio maana wakampiga unategemea serikali tufanyaje “alihoji Mwambene.
          
           Kauli hiyo ya Mwambene inatafsiriwa tofauti na wadau wa Masuala ya Habari kwani kuzungumza huku kunazidisha maswali mengi kutokana na Idara ya habari maelezo ndio inayowasimamia Waandishi pamoja na Magazeti.
   
             Kwa Upande wake Mwandishi ambaye anashutumiwa na Mwambene Josephati Isango wa Gazeti la Tanzania Daima,wakati alipokuwa anafanyiwa mahojianao maalum na Mwandishi wa Mtandao huu jana jijini dare s Salaam,ambapo alisema kwa sasa anajipanga kwenda mahakamani kumburuza mahakamani Cp Chagonja,Polisi watatu waliompiga pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

          “Nasahivi nawasiliana na Wanasheria wangu watatu jinsi ya kwenda mahakamani kuwashitaki polisi watatu,Cp Chagonja,waziri mkuu mizengo Pinda ambaye ametoa kauli ya pigwa tu Bungeni nafanya hivi kupata haki ya kwetu sisi waandishi Habari”alisema Isango   

No comments: