Kampuni
ya mawasiliano ya simu za mkononi ya
TIGO Tanzania leo imekuwa kampuni ya kwanza duniani kuzindua huduma inayowapa
watumiaji wa tigo pesa fursa ya kupata gawio la faida kwenye account zao
kulingana na kiwango cha fedha kilichopo.
Akitangaza
huduma hiyo ya TIGO WEKEZA meneja mkuu wa Tanzania DIEGO GUTIEREZ amesema kuwa
zaidi ya wateja million 3.5 wa tigo pesa watanufaika na malipo hayo ambayo
yatatolewa mara nne kwa mwaka kila baada ya miezi mitatu.
Ameongeza
kuwa Hii ina maana kuwa tigo pesa haitakuwa tena huduma ya kupokea na kutuma pesa tu kama ilivyo hivi sasa bali
ni njia mojawapo kujipatia kipato cha ziada kupitia huduma ya tigo wekeza.
Ikumbukwe
kuwa wiki iiyopita kampuni hiyo ilitangaza kutoa gawio la shilingi billion
14.25 kwa wateja wake wa tigo pesa kutoka katika mfuko wake wa fedha za account
ya tigo pesa kitendo kilichoifanya kuwa kampuni ya kwanza duniani ya simu kutoa gawio kupitia huduma ya kutuma
na kupokea pesa ambapo gawio hilo liliidhinishwa na benk kuu ya Tanzania (BOT).
Kwa
maelezo ya meneja mkuu wa tigo amesema kuwa watumiaji wa tigo pesa watakuwa na
nafasi ya kuchagua iwapo watataka kupokea au kuchangia gawio hilo kwa taasisi
isiyo ya kiserikali,kutokana na sababu zao binafsi za kiutamaduni au
kiimani,ili kupata huduma hiyo mteja atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno
WEKEZA kwenda namba 15514 ambapo atapata maelezo zaidi.
Aidha
katika hatua nyingine mkuu wa shirika linalosimamia huduma za mawasiliano ya simu
duniani (GSMA) TOM PHILLIPS ameitumia tigo salamu za pongezi akisema kwamba
huduma hii mpya ni mfano mwingine wa jinsi ambavyo secta ya mawasilano
inachangia katika kuleta maendeleo ya kijamii na kifedha katika jamii.
No comments:
Post a Comment