Habari zilizotufikia mda huu zinasema Mwanasheria mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya zanzibar OTHAMAN MASOUD OTHAMAN amefukuzwa kazi na nafasi yake imejazwa mara moja na Naibu mwanasheria Mkuu SAID HASSAN SAID .
DURU za kisiasa zinasema kufukuzwa kazi huko kwa mwanasheria mkuu huyo kunatokana na yeye kupinga baadhi ya vipengele kwenye Rasimu ya Katiba iliyopondekezwa na Bunge Maalum la Katiba,
Sababu hiyo ndio ikamfanya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar DK SHEIN kumfukuza kazi kwa kile anachokiona ni ameihabisha serikali yake.
Wachambuzi wa masuala ya Mambo wanasema kitendo cha kufukuzwa kwa mwanasheria huyo kitaipasua hali ya siasi visiwani humu kutokana na chama cha mapinduzi ccm kuonekana kuvaa vazi la udikteta na kushindwa kuacha uhuru wa maoni wa kuchagua na kukataa.
Rais Shein amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.
Mhe. Said Hassan Said ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na uteuzi huo umeaza rasmi leo 7, Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu.
Uteuzi wa Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
No comments:
Post a Comment