Wednesday, October 8, 2014

HABARI NJEMA KUTOKA FINCA LEO

 Kaimu Afisa Mwendeshaji Mkuu wa FINCA Tanzania ,Bwan.Daniel
Mhina akifafanua zaidi kuhusiana na Faida za akaunti za akiba za Finca
kuwa ni nyingi,ikiwa ni pamoja na urahisi wa kufungua na kuendesha
akaunti,taratibu za kufungua akaunti zina mahitaji madogo,kutoa na
kuweka pesa bure kwenye matawi yote nchini na usalama wa fedha za mteja
kupitia mfumo wa bayometriki unaotumiwa na benki hiyo.Bwan Daniel
alisema kuwa kupitia matawi ya FINCA inahudumia wateja zaidi ya 120000
ambao wanahudumiwa na zaidi ya wafanyakazi 700 nchini. pichani shoto ni
Mkuu wa Huduma za Kibenki wa FINCA,Bwa.Gershom Mpangala pamoja na Meneja
tawi la Magomeni Bwa.Cassian Clovis.
Mkuuwa Huduma za Kibenki wa FINCA,Bwa.Gershom Mpangala akizungumza mbele ya
Waandishi wa Habari (hawapo pichani),kuhusiana na taasisi hiyo ya
Kifedha kuzindua kampeni yake mpya  iliyojulikana kwa jina la Fika na
Finca,kampeni inayolenga kuwafikia Watanzania wote kupitia huduma za
kibenki na kuwasaidia kutimiza malengo ya kimaendeleo
waliyojiwekea,Mkutano huo umefanyika kwenye moja ya Ofisi zao zilizopo
Mwembechai Jijini Dar.Pichani kati Kaimu Afisa Mwendeshaji Mkuu wa FINCA
Tanzania ,Bwan.Daniel Mhin pamoja na Meneja tawi la Magomeni
Bwa.Cassian Clovis


FINCA Tanzania leo imezindua "FIKA NA FINCA" kampeni ambayo inalenga kuwafikia watanzania wote kupitia huduma za kibenk na kuwasaidia kutimiza malengo yao ya kimaendeleo waliyojiwekea.

Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam leo mkuu wa huduma za kibenki wa finka Bwa.Gershom Mpangala amesema kuwa mteja kwa mara ya kwanza sasa anaweza kupata mkopo wa hadi shilingi million 150 ndani ya siku tano tu.ambapo pia FINCA itatoa mkopo wa kilimo kwa wakulima hasa wale walioko katika maeneo ya kijijini na mkopo wa elimu kusaidia wamiliki wa taasisi za elimu na wale wamaohitaji kulipia ada za watoto na ndugu zao.


No comments: