Friday, October 10, 2014

HABARI ILIYOTIKISA JIJI--HUJUMA NZITO KWA SAMWELI SITTA,JINA LA MJUMBE WA NCCR LAKUTWA KWA WALIOPIGA KURA,MJUMBE AZIMIA MBELE YA WANAHABARI AKIELEZEA ANAVYOTISHIWA MAISHA

Na Karoli Vinsent


       HUJUMA alizofanya Aliyekuwa mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta wakati wa Kupata Thelutihi 2 kwa Upande wa Zanzibar ili kupitisha Rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Bunge,sasa hujuma hizo zaanza kufichuka,

       Hujuma hizo zimeibuka leo  Baada ya Chama Cha NCCR mageuzi kuibuka na kufichua hujuma iliyofanywa na Samwel Sitta kutokana na kumuorodhesha Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi Zanzibar Ndugu Haji Ambar Khamis kuwa Miongozi mwa wajumbe walioshiriki kupitisha katiba hiyo iliyopendekezwa huko yeye akuwepo wala akushiriki vikao hivyo.

         
        Hayo yameibuliwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Mbatia alisema chama hicho kilipopata taarifa za kuorodhesha kwa Mjumbe huyo kuhusu kupitisha Rasimu ya Bunge ndipo wakafanya uchunguzi ikiwemo na kumwita Ndugu Haji Ambar Khamisi ili kupata ukweli.
      
        “Tumechunguza na Kubaini kwamba Ndugu   Haji Khamis,ametuthibitishia kwa dhati kwamba hakuwahi kushiriki katika kuandaa wala kupitisha katiba iliyopedekezwa tangu bunge hilo liliporejea kwa mara ya pili tarehe 05 agosta 2014.”

        “ Na kitendao cha kuandika jina la kiongozi wetu wa Taifa katika katiba iliyopendekezwa bila ridhaa yake ni ulaghai uliokithiri kwa watanzania na Dunia kwa ujumla kwani kitendo hicho ni cha udhalilishaji kwa yeye binafisi,Familia yake chama chetu pamoja na viongozi wanachama wote wa Umoja wa kutetea katiba ya wanachi UKAWA na watanzania”Alisema Mbatia.
     
          Mbatia alizidi kusema chama hicho kimeamini kitendo hicho kimefanywa kwa makusidi na Viongozi wakuu wa Bunge Maalum la Katiba ili kukidhi haja zao Binafsi na kulaghai umma wa Watanzania na kusema ni ishara hatarishi kwa usalama wa Taifa letu kwani kitendo hicho kinaweza kusababisha machafuko.
        
       Aliongeza kuwa Uongozi wa NCCR-Mageuzi umepokea katiba iliyopendekezwa kwa Fedheha na Mshtuko mkubwa na kuamini kuwa kuna mkakati mbaya wa kusambaratisha chama hicho kinachokua kwa kasi nchini.
          
        Aidha,Mbatia alisema kwa sasa Chama chake hakitaweza kuvumilia uongo na Uzushi aliufanya mwenyikiti wa Bunge Maalum La katiba katika kupata Thelusi 2 kwa upande wa Zanzibar kwa kufoji wajumbe ambao hawakuwepo kwenye bunge hilo na kusema kwa sasa chama hicho tayari kimewasiliana na wanasheria ili kwenda mahakamaini ili hujuma hiyo igundulike.
        
           Kwa upande wake ndugu Haji Ambar Khamis alisema anashangaa sana kwa kutajwa katika wajumbe walioshiriki kupiga kura kuipitisha rasimu ya bunge na kusema hajawai kuwepo wala kushiriki katika bunge hilo.
      
          “Yaani nashangaa sana maana nimekuwa siishi kwa raha napigiwa simu za vitisho kutoka sehumu mbalimbali na kusema ukweli jamini mimi sijawai kuwepo kwenye Bunge la katiba tangu tulivyosusia vikao hivyo na huu umoja wetu wa UKAWA nashangaa sana leo natajwa mimi kuwepo jamani huu ni uongo mkubwa sana mimi sikuwepo”alisema Khamisi
    
          Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Wakati Haji Ambar Khamisi akiwa akijielezea alishindwa kabisa na kuanza kulia na kusema Familia yake ipo katika hali mbaya pamoja na  yeye kutokana na hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar kuanza kuchafuka na uwenda familia yake ikauliwa.
       
           Baada ya kusema maneno hali ikazidi kuwa mbaya na akapata mshutuko huku kikao hicho na Waandishi wa Habari kikasimamishwa

na kumkimbiza Haraka Hospitali ya Amana iliyoko Jijini hapa kupata Matibabu.

       
            Baada ya Hali hiyo kutokea ndipo Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia aliitaka Serikali impe ulinzi Mjumbe huyo huku ikizingatia undani wa suala lenyewe na akakumbushia Mauaji ya Kikatili na yakinyama aliyofanyiwa aliyekuwa mjumbe wa iliyokuwa tume ya marekebisho ya katiba Marehemu Dkt Edmund Mvungi na kusema uwenda unyama huo ukamkuta makumu huyo mwenyekiti. 

No comments: