Mkurugenzi wa uwezeshaji wa LHRC Bi EMELDA URIO akizungumza na wanahabari leo Jijini dar es salaam kuushoto kwake ni mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho HELLEN KIJO BISIMBA. |
Ikiwa dunia leo inaadhimisha siku ya kupinga adhabu
ya kifo Duniani Kituo cha Sheria na Haki
za binadamu nchini LHRC kimeitaka serikali na mamlaka husika kuondoa kabisa
adhabu hiyo ikiwa ni pamoja na kufuta vipengele na sheria ambazo zinaelekeza
adhabu hiyo na badala yake kuweka mbadala wa adhabu nyingine kama kifungo cha
maisha kwani kuendekea kuwepo kwa adhabu hiyo ni ukiukwaji wa haki ya binadamu
ya kuishi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Jijini Dar es
salaam Mkurugenzi wa uwezeshaji wa LHRC Bi EMELDA URIO amesema kuwa adhabu ya kifo inaondoa uwezekano
wowote wa mkosaji kujirekebisha,huku akisema kuwa ni adhabu ya kikatili isiyo ya kibinadamu
hivyo haistahili kuendelea kuwepo kwenye sheria za nchi.
Mkurugenzi huyo anasema kuwa adhabu ya kifo pia inavunja misingi ya tamko
la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948 ambalo linasema kila mtu ana
haki ya kuishi na pia ni marufuku kutoa adhabu ya kikatili kama kifo.
Aidha amesema kuwa Tanzania inapaswa kujifunza
kutoka kwa mataifa mengine duniani ambayo hayatekelezi adhabu hii ya kifo na
badala yake kutoa adhabu mbadala kama kifungo cha maisha na kazi ngumu kwa
watuhumiwa wa mauaji ili kulinda haki hii ya msingi ya kuishi.
Aidha amesema kuwa bado kwenye katiba pendekezwa
iliyowasilishwa kwa mh Rais inaonyesha kuwa adhabu hiyo bado ipo ambapo amesema
wanamtaka rais kufanya mipango ya kuondoa vipengele hivyo kwani ni kinyume na
haki za binadamu.
Katika hatua nyingine Bi EMELDA amesema kuwa
harakati za kupinga adhabu ya kifo hazimaanishi kuwa ni kutetea uhalifui hasa
mauaji ila ukweli ni kwamba hakuna ushahidi kuwa uwepo wa adhabu hiyo unaweza
kupunguza uhalifu na badala yake ni bora kukawa na adhabu nyingine mbadala nje
ya adhabu hiyo.
Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani kama ,CHINA,IRAN,KOREA
KASKAZINI,NA MAREKENI ambazo bado zinaruhusu na kutekeleza adhabu ya kifo
katika sheria zao.ampapo nchini Tanzania adhabu hiyo ipo kwa mujibu wa sheria
ya kanuni za adhabu,sura ya 16 ya sheria za Tanzania,kifungu cha 197 kinachoeleza
kwamba MTU YOYOTE ALIYEPATIKANA NA HATIA YA KUUA ATAHUKUMIWA ADHABU YA KIFO.
No comments:
Post a Comment