Saturday, October 18, 2014

HABARI KUBWA LEO JIJINI--HISTORIA MPYA UKAWA,SOMA WALICHOKITANGAZA LEO

Makamu mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA profesa ABDALA JUMBE SAFARI akiwasili makao makuu ya CUF tayari kuzungumza na wanahabari leo
 Umoja wa katiba ya wananchi Tanzania UKAWA leo umetangaza rasmi kuanza mashirikiano ya vyama vyao katika chaguzi mbalimbali zijazo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wamauondoa utawala ulioko madarakani ambao wameutaja kuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya watanzania walio wengi.

        Akizungumza na wanahabari leo makao makuu ya chama cha CUF mwenyekiti mwenza wa UKAWA profesa IBRAHIM LIPUMBA amesema kuwa muungano  wa ukawa sasa umekua na kufikia hatua nzuri hivyo wameamua kufanya jambo hilo la kihistoria kwa maslahi ya watanzania wengi ambapo sasa wataanza kusimammisha mgombea mmoja katika kila chaguzi wakianzia na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mwenyekiti wa CUF profesa IBRAHIMU LIPUMBA akiwa na katibu mkuu wa CHADEMA Dk WILBROD SLAA wakiwasili katika mkiutano huo
  “ukawa tumeamua kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na tutashiriki kama UKAWA,tutasimamisha wagombea kwa nchi nzima kila eneo kwa umoja wetu,wagombea wetu watateuliwa kwa kufwata vigezo ambavyo vyama tutakubaliana tumeklubaliana na pia kwa maoni ya wananchikatika eneo husika”amesema LIPUMBA.

         Aidha amesema kuwa muungano huo utaendeleo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo umoja huo watasimamisha wagombea wa udiwani,ubunge na hata urais kwa umoja wao huku akisema lengo ni kuwa na nguvu kubwa ya kuwaondoa aliowaita mafisadi CCM katika utawala wa Tanzania.
Umoja huo umetangaza kuwa utafanya mkutano mkubwa jijini Dar es salaam terehe 26 mwezi wa 10 ambapo katika mkutano huo ndipo watasain makubaliano rasmi mbele ya wanachama wao juu ya ushirikiano wao huo.



         Katika hatua nyingine UKAWA wamesema kuwa wataipinga kwa ngivu zote katiba pendelezwa iliyotokana na bunge maalum la katiba kwa kile walichoita kuwa ni katiba haramu na haina uhalali kisheria huku wakiwataka watanzania kutokuikubali na badala yake kuipigia kura ya hapana katiba hiyo

          Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA unaundwa na vyama vya upinzani ambavyo viilitoka nje katika bunge la katiba kwa madai kuwa maoni ya wanachi yamechakachulkiwa ambavyo vyama hivyo ni CUF,CHADEMA,NCCR MAGEUZI pamoja na NLD

No comments: