Friday, October 17, 2014

HII HAPA TAARIFA KUTOKA KAMATI KUU YA CCM INAYOKUTANA DODOMA

Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya
ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza juu ya kikao cha
Halmashauri Kuu
ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku
ya
kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini
ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya
Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea
kimapato na
kiuchumi. 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na kiuchumi.
Sera hiyo inalenga kuwa muongozo wa kuifanya CCM ianze kuzitumia rasilimali zake kuzalisha ili iweze kujitegemea kiuchumi.
Kama inavyofahamika CCM ina rasilimali nyingi wakiwemo wanachama wake, viwanja na majengo ambavyo kwa pamoja vkitumika vizuri vitasaidia kukifanya chama kuondokana na utegemezi wa ruzuku na badala yake kujitegemea.
Aidha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wagombea kwa nafasi za Uenyekiti wa CCM katika wilaya mbili pamoja na wagombea Ujumbe wa NEC katika wilaya tatu zilizokuwa na nafasi wazi.

WALIOTEULIWA KUGOMBEA UENYEKITI WA WILAYA NI;-

Wilaya ya Njombe:-
Ndugu Edward Pius Mgaya
Ndugu Vallence Mtenzi Kabelege
Ndugu Betram Simon Ng’imbudzi
Wilaya ya Misenyi:-
Ndugu Sosthenes Rweyemamu Kabandwa
Ndugu Said Ibrahim Seruh
Ndugu Erica Kiiza Stephen

WALIOTEULIWA KUGOMBEA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NI:-
Wilaya ya Tandahimba:-
Ndugu Lutavi Abdula Suleman
Ndugu Malela Mohamed Chibwana
Ndugu  Nanyundu Ally Salum
Wilaya ya Mkuranga:-
Ndugu Ally Mohamed Msikamo
Ndugu Maulid Hamis Zowange
Ndugu Wakati Nassoro Mtulia
Ndugu Zawadi Ally Kilapo
Wilaya ya Njombe:-
Ndugu Christian Marcus Fwalo
Ndugu George Benedict Mng’ong’o
Ndugu Oscar Michael Msigwa
Ndugu Justin Nusulupia

Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,    
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
17/10/2014







No comments: