Katibu mkuu wa Chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA dk WILLBROD SLAA akizingumza na wanahabari jijini Dar es salaam mapema leo |
Chama cha democrasia na maendeleo chadema leo kimetagnaza
rasmi kuanza kwa kampeni ya siku ishirini nchi nzima ya kuzunguka kuwahamasisha
watanzania kuipinga kwa nguvu moja rasimu ya katiba iliyopendekezwa na bunge
maalum la katiba kwa kile walichooita kuwa ni kukosa uhalali wa kisheria na
kujawa na ukiukwaji mkubwa wa kisheria tangia mchakato huo kuanza.
Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam
wakati akisoma maadhimio ya kamati kuu ya chama hicho katibu mkuu wa CHADEMA dk
WILBROD SLAA amesema kuwa kamati kuu imejiridhisha kuwa mchakato wa katiba
katika hatua zake zote ulitawaliwa na nia mbaya iliyokuwa na lengo kuu la
kuhakikisha kuwa hakuna mabadiliko makubwa na ya maana yatakayofanyika kwenye
mfumo wa kikatiba na kiutawala ambao umekuwepo nchini kwa miaka zaidi ya hamsini.
Dk slaa amesema kuwa mkutano huo uliokaa kwa siku
mbili jijini Dar es salaam umekuja na maadhimio mengi lakini kubwa likiwa ni
kuwahamasisha wananchi kupiga kura ya hapana kwa katiba pendekezwa pamopja na
kuwahamasisha kujitpokeza katika chaguzi za serikali za mitaa zitakazokuja.
Akitaja mambo ambayo yameufanya mchakato wa katiba
kutokuwa na uhaali kwao ni pamoja na uteuzi wa wajumbe ambao wengi amesema
walichaguliwa kwa lengo la kuwasaidia ccm,lugha chafu ndani ya bunge,bunge
maalum la katiba kugeuzwa tume na kuanza kukusanya maoni upya,muda wa
kuwasilishwa kwa taarifa na kamati mbalimbali ulifupishwa,utaratibu wa kupiga
kura kifungu kwa kifungu ulibadilishwa,pamoja na wajumbe waliokuwa nje ya bunge
kupiga kura.
Kutokana na mambo hayo chama hicho kimeamua kwenda
nchi nzima kuwahamasisha watanzania kupiga kura ya hapana kwa mchakato huo
ambapo wanaenda kwa mafungu ambapo kesho baraza la wanawake BAWACHA wanaanzia
MWANZA na baadae kufwata baraza la vijana na wengine.
No comments:
Post a Comment