Kampuni ya rangi ya berger paints international LTD imeshauri serikali
kupunguza kodi ya viwanda katika ukuaji wa uchumi na viwanda nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam kurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo MEHBOOD BHARWAN
amesema kumekuwa na utozaji mkubwa wa kodi ikiwemo kulipa kodi mara tatu zaidi
ya zamani hali ambayo amesema inapelekea kufa kwa viwanda nchini.
Aidha BHARWAN amesema kuwa BERGER
PAINTS ni moja inayozalisha bidhaa zenye ubora zaidi ambapo kampuni hiyo
inajihusisha na utengenezaji wa rangi ya (robialak)yenye matawi mbalimbali hapa
nchini ikiwemo Dodoma na arusha.
Mkurugenzi huyo ameiomba serikali
kuangalia mfumo wa ulipajhi kodi upya kwa kupunguza idadi ya kodi inayotozwa
kwa sasa na pia kurejkebisha miundombini hususani barabara ili bidhaa ziweze
kufika sehemu husika kwaq muda muafaka kwani secta hiyo ndio mhimili katika
ukuaji wa uchumi wa taifa.
No comments:
Post a Comment