RAIS Jakaya Kikwete ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM,amekuwa mtu wa kwanza kwa upande wa Chama chake Kumpongeza,Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Demokrasina na Maendeleo CHADEMA BAWACHA,Halima Mdee.
Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe Chadema,amepewa Pongezi hizo na Rais Kikwete leo Jijini Dar Es Salaam wakati alipokuwa anafufungua barabara kati ya mwenge hadi kawe ,ambapo wakati anahutubia wananchi rais kikwete alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mdee.
“Natumia Nafasi hii kumpongeza sana Mwanamama Halima Mdee kwa kuchaguliwa kwenye nafasi ya Umoja wa Wanawake ndani ya Chadema,tena nasikia unataka kuonana na mimi namwambia karibu tena namngojea”alisema Rais Kikwete.
Kwa Upande Halima Mdee mwenyewe mara baada ya kupongezwa na Rais Kikwete akusita kutoa lawama zake kwa Viongozi wa mkoa wa Dar Es Salaam kwa kushindwa kumtaharifu kwake juu ufunguzi wa barabara hiyo na kusema ofisi ya mkuu wa mkuu wa mkoa ilifanya makosa kwani barabara hiyo ipo katika Jimbo lake.
“Kikweli nasikitika sana yaani wala sikupewa hata taarifa rasmi juu ya kuzinduliwa barabara hii,licha kusikia kwa watu,ni jambo lakushangaza sana mimi kama mbunge ninatakiwa nipewa taarifa hili ni jimbo langu na sijui kwanini viongozi wa mkoa Dar es Salaam wanashindwa kunipa taarifa ?”alihoji Mdee.
Licha ya Mdee kutoa malalamiko hayo,Mwandishi wa Mtandao huu alimshudia Mbunge huyo akiende kwenye Jukwaa la wageni Rasmi ambapo ndipo alipokaa Rais Kikwete huku nafasi yake kutokuwepo na kuwaacha wananchi pamoja na waandishi wa habari wakishangaa hali hiyo,ila bahati nzuri alipofika jukwaani kulikuwepo na nafasi moja ambayo hakutakiwa kukaa mbunge huyo lakini yeye alikwenda na kuketi, kwa maana yake Halima mdee akuwa amepewa mwaliko katika uzinduzi huo
No comments:
Post a Comment