Thursday, October 9, 2014

MICHEZO--LSA YAANZA VYEMA LIGI DARAJA LA NNE LINDI



TIMU ya Lindi Soccer Academy (LSA), juzi imeanza vema michuaano ya soka ya Ligi Daraja la Nne Manispaa ya Lindi, baada ya kuilaza Lindi FC mabao 2-1 katika pambano kali la ufunguzi kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi.
Akizungumza baada ya filimbi ya mwisho ya pambano hilo, Mkurugenzi wa LSA, Hafidh Karongo, alisema kikosi chake kilionesha soka la hali ya juu katika mechi yake hiyo ya kwanza, licha ya upinzani mkali kutoka kwa Li
di FC.
Wafungaji wa LSA katika mechi hiyo walikuwa ni Mohamedi Riwadi ‘Muddy Drogba’ akitumia vema pasi ya nahodha wake Shaffih Maulidi, huku bao la ushindi likifungwa na Abdalah Ismail akiunganisha ‘free kick’ Hamdani Sarahani ‘Mido.’
Bao la kufutia machozi la Lindi FC lilifungwa na Michael David dakika ya 40.
Karongo aliwapongeza nyota wake wa LSA kwa aina ya upiganaji waliouonesha katika pambano hilo, na kwamba mwanzo mwema walioupata unawapa morali ya kuhakikisha wanashinda mchezo mmoja baada ya mwingine.
“Hii ni mara yetu ya kwanza kushiriki michuano ya Ligi Daraja la Nne Manispaa ya Lindi na lengo la pamoja ni kufanya vizuri ikiwezekana kutwaa ubingwa. Mwanzo huu unatupa zaidi ya nguvu ya kufanya makubwa mashindanoni,” alisema Karongo.
Kwa mujibu wa Karongo LSA inashuka tena dimbani leo Ijumaa kukipiga na Magereza FC ambayo nayo juzi katika ufunguzi iliichapa timu yenye mbwembwe nyingi na tambo nyingi ya Stand Warriors bao 1-0 shukrani kwa mkwaju wa penalti wa God Mkoma

No comments: