Monday, October 6, 2014

SERIKALI YAIPONGEZA BODI YA UKAGUZI WA MAHESABU NBAA

SERIKALI imeipongeza bodi ya uhasibu na ukaguzi wa mahesabu (NBAA) kwa kuweza kujenga kituo cha taaluma ua uhasibu ambacho kitatumiwa kusaidia kupunguza gharamza za uendeshaji  wa bodi hiyo.

       Akizungumza katika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam katika mahafali ya 36 ya NBAA naibu waziri wa fedha mh. KIGHOMA MALIMA amesema kuwa kujengwa kwa kituo hicho kutapunguza gharama za uendeshaji wa bodi ususani katika masuala ya mitihanai,semina na mafunzo mbalimbali na vile vile kama chanzo cha mapato.


      Waziri malima alisema kuwa NBB imeamua kufanya mahafali hya kataika kituo hiki ili wadau mbalimbali waweze kujionea wenyewe maendeleo ya kituo hiki,kituo cha kitakuwa na huduma mbalimbali zikiwemo kumbi za mikutano ,huduma za hoteli na malazi ,huduma za mazoezi na nyinginezo

      “Serikali  itaendelea kusaidia NBAA katika kukamilisha ujenzi wa kituo hiki ,naelewa kuwa ujenzi unaendelea vizuri na kuwa kituo kinatarajiwa kukabidhiwa kwa NBBA hivi karibuni”alisema waziri malima.

         Aidha waziri malima alisema kuwa serikali kupitia wizara ya fedha itaendelea kushirikiana na NBAA katika mambo mbalimbali hasa yale yanayolenga kuboresha fani ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu hapa nchini ,pia  itaendelea kusaidia bodi katika kutekeleza majukumu na malengo yake hii ni pamoja na kuendelea kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa NBBA ili kuwapa motisha zaidi wa kufanya kazi kwa moyona kwa ufanisizaidi.

         Naibu waziri huyo ameitaka NBAA kushirikiana na bodi nyingine za nje kwa ukaribu zaidi ili iweze kujifunza kwa wengine kwa kuwa kila siku kuna mambo mapya ya kujifunza .
Waziri malilma alihitimisha kwa kuwapongeza wahitimu wote ambao wametunukiwa vyeti na baadhi yao kupewa zawadi mbalimbali kufanya vizuri zaidi katika masomo:nafahamu kwamba kuna wengine wengi


No comments: