Monday, October 6, 2014

KIINGILIO TAIFA STARS, BENIN 4,000/-


Kiingilio cha mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Benin (Squirrels) itakayochezwa Jumapili Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni sh. 4,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho katika mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa ni kwa ajili ya viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu. Kwa washabiki watakaokaa jukwaa la VIP B kiingilio ni sh. 10,000. Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo ni za elektroniki ni

Viti vya VIP A na C hakutakuwa na viingilio, na badala yake vitatumika kwa ajili ya wageni maalumu watakaolikwa kutoka katika madhehebu ya dini za Kikristo na Kiislamu.


Mechi kati ya Taifa Stars na Squirrels itaanza saa 11 kamili jioni, na itatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo, amani, udugu na ushirikiano kati ya timu za taasisi za dini ya Kiislamu na Kikristo itakayochezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri.

Wakati huo huo, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini leo (Oktoba 6 mwaka huu) kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi dhidi ya Benin.

Timu hiyo chini ya Kocha Mart Nooij kesho (Oktoba 7 mwaka huu), Jumatano (Oktoba 8 mwaka huu) na Ijumaa (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji Thomas Ulimwengu kutoka timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) na kiungo Mwinyi Kazimoto kutoka timu ya Al Markhiya ya Qatar tayari wametua nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars.

Naye mshambuliaji Juma Liuzio kutoka timu ya Zesco ya Zambia anawasili nchini kesho (Oktoba 7 mwaka huu) mchana kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola kupitia Nairobi.
ajili ya mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 jioni.

Kwa mujibu wa Kocha Nooij, timu hiyo itakuwa na vipindi (sessions) 11 vya mazoezi kabla ya kucheza na Benin (Squirrels). Stars itafanya mazoezi asubuhi na jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo baadhi yatafanyika Uwanja wa Taifa, na mengine kwenye uwanja mwingine.

Wachezaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Mwinyi Kazimoto anayechezea timu ya Al Markhiya ya Qatar wanawasili nchini kesho (Oktoba 6 mwaka huu).


Naye mshambuliaji Juma Liuzio anayechezea timu ya Zesco ya Zambia atawasili nchini keshokutwa (Oktoba 7 mwaka huu) kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola.

No comments: