Monday, October 13, 2014

TAARIFA MUHIMU TOKA CHADEMA ASUBUHI HII


TAARIFA KWA VYOMBO

KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CHAMA

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inatarajiwa kukutana jijini Dar es Salaam katika kikao maalum cha siku mbili, tarehe 14-15 Oktoba, 2014.
Pamoja na masuala mengine, Kamati Kuu ya Chama itajadili mambo mbalimbali katika agenda zifuatazo;
·       
       - Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba
·       
       -Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji
·        
     -Operesheni za Ujenzi na Uimarishaji wa Chama
·        
       -Taarifa ya Fedha

      Kikao hicho kitatanguliwa na hotuba ya ufunguzi.

Imetolewa leo  na;

     Tumaini Makene


Mkuu wa Idara ya Habari- CHADEMA


No comments: