Friday, October 10, 2014

TIGO WAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA KWA STAILI YA AINA YAKE

Mkuu wa idara ya Huduma kwa wateja, Ndugu Zaeem Khan akikabidhi kadi za kipaumbele kwa wateja walio hudhuria hafla hiyo.

Kampuni ya mawasiliano ya TIGO TANZANIA imeadhmisha wiki ya huduma kwa mteja ndani ya kampuni hiyo kwa kuwapa nafasi wateja wake nafasi ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika ndani ya kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuwatembeza wateja wake katika vitengo mbalimbali ndani ya kampuni hiyo.ikiwa ni pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali wateja wake waliopata nafasi ya kutembelkea maduka ya tigo. hizi hapa ni baadhi ya picha za matukio hayo


 Wateja wakisikiliza mazungumzo mojakwamoja Baina ya mteja na muhudumu wetu katika kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu (Callcenter)


Mkuu wa Idara ya Huduma kwa wateja Ndugu Zaeem Khan akitoa zawadi ya Sim kwa mteja wetu wa Tigo katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.



Wateja waliopata nafasi ya kutembelea kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu (Callcenter) wakipata maelekezo kuhusu huduma za Tigo.
 

Picha ya pamoja ya Wafanyakazi  na wateja wa Tigo waliotembelea kituo cha Huduma kwa wateja kwa njia ya simu (Callcenter).
 

No comments: