Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh.Dkt. Christine Ishengoma akisalimiana na Mkurugenzi mkuu wa Tigo kanda ya kusini Bw. Jackson Kiswaga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kifurushi kipya cha tigo cha welcome pack mkoani Iringa, kifurushi hicho kitamwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakiak 20, mb175,sms bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tigo ya zindua huduma mpya ya
‘Welcome Pack’
.Tigo Tanzania leo imezindua kifurushi kipya cha
‘Welcome Pack’ ambayo itawezesha wateja wake kupata huduma ya intanet, SMS, na kupiga
simu kwa bei nafuu. Uzinduzi wakifurushi hichi pia inaenda sambamba na kampeni maalum
yenye nia ya kuwa elimisha watu na kuwapa fursa ya kushuhudia bidhaa na huduma mbalimbali
itakayofanyika katika mikoa 10 nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hii iliyofanyika
katika Uwanja wa Sokoine mkoani Iringa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Dk.
Christtine Ishengoma aliipongeza sana mchango wa Tigo katika kuleta maendeleo kwa
watu wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kwa kuwekeza katika sekta ya mawasiliano ambayo imekuwa kama kichocheo kikubwa katika kuleta maendeleo
ya kiuchumi na kijamii kwa watu hususan wa
mikoani.
“Suala la kwamba kifurushi cha Welcome Pack itawapatia
Nwananchi fursa ya kupata dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 zakuperuzi katika
intanet, SMS zisizo na kikomo na Tsh 500 katika akaunti yake mpya ya TigoPesa,
yote hayo kwa Tsh 1000 kama gharama ya kununulia
laini ya simu itawapatia wateja nafasi nzuri yakuwasilia na zaidi na kwa gharama nafuu,”alisema Dk. Ishengoma.
“Napenda kuchukua nafasi hii kutoarai kwa wananchi wote
wa Iringa kuchangamkia kifurushi hiki maalum
kutoka Tigo kwaajili ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii hapa mkoani
nap engine. Tumieni muda wa maongezi, intanet, SMS zabure kuwezesha miamala ya kibiashara
na kupata elimu ya kibiashara mtandaoni, vitu ambavyo mwisho wa siku vitawasaidia
kuongeza uzalishaji na kupata masoko ya kibiashara,” alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Dk. Ishengoma pia alisifia kampuni ya Tigo kwa hatua yao
ya kuanzisha Basi la Kidijitali la Tigo lenye uwezo wakuwapatia Watanzania elimu
kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zito lewazo na kampuni hiyo kama Tigo Kilimo,
Tigo Bima, TigoPesa, Application ya Hesabati kwa wanafunzi wa sekondari, na
Facebook ya Bure kwa Kiswahili.
“Ni dhahiri kwamba ujanawazo hili la kibunifu litasaidia
kuongeza elimu ya kidijitali kwaWatanzania hasahasa wale wa vijijini, ambayo moja
kwamoja inachangia katika ufanikishwaji wadira ya kampuni yenu yakuwezesha maisha
yakidijitali nchini,” alisema Dk. Ishengoma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda za Juu Kusini,
Joseph Kiswaga alisema kwamba kampuni ya Tigo inayofuraha kutangaza uzinduzi rasmi
wa kampeni ya Welcome Pack ambayo itawazawadia wateja wa Tigo watakaojiungana mtandao
huo kwa mara ya kwanza kwa kununua laini za Tigo.
Alisema, “Kampeni ya Welcome Pack itakuwepo kwa muda wamie
zimi tatu, ambapo misafara zaidi ya 70 ikiwemo basi la Tigo la Kidijitali litatembelea
miji 70 na vijiji Zaidi ya 100 ndani ya mikoa 10 tofautii kiwemo Mbeya, Iringa,
Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Mtwara.”
“Misafara hii yataambatana na tamasha la muziki katika
kila siku ya mwisho wamsafara utakao fanyika kila Jumapili. Wasanii wa Bongo
Fleva watakaotoa burudani ni pamoja na Profesa J, Joh Makini, Shah, Mheshimiwa
Temba na Chege, Madee na Izzo Business. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwa karibisheni
nyote,” alimalizia kwa kusema Kiswaga.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment