JUMUIYA ya Vijana na Wanawake wa Chama cha Wananchi CUF kimetangaza uchaguzi wa ngazi za matawi,kata,wilaya kwa ujumla ambapo mpaka mwishoni mwa Novemba mwaka huu chama hicho kitakuwa kimekamilisha uchaguzi kwa wilaya zaidi 80 kwa Zanzibar na Tanzania bara,
Na uchaguzi wenyewe utafanyika kuanzia tarehe 15 mwezi 11 mwaka huu hadi tarehe 22 mwezi 11 mwaka huu ambapo Jumuiya ya Vijana kutoka chama hicho pamoja na Jumuiya ya Wanawake zitakuwa zimekamilisha chaguzi zake za ngazi ya Wilaya.
Akitangaza Uchaguzi huo leo Jijini Dar Es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi CUF(JUVICUF),Hamidu Bobali amesema uchaguzi huo utakuwa huru na ukizingatia suala zima la Demokrasia na kutoka fursa kwa vijana na wanawake kuomba nafasi mbalimbali za uongozi kwa ajili ya kuwakilisha Jumuiya zao katika ngazi za juu za maamuzi katika chama hicho.
Akaongeza kuwa uchaguzi huo utazingatia katiba na kanuni ya chama hasa kwa upande wa vijana ambapo umri wa mgombea ni hutakiwa kuzidi miaka 35, na jumuiya ya wanawake sifa kubwa ni kuwa mwanamke mwanachama umri ni kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Vilevile Bobali alizidi kusema form za kuomba nafasi ya Mwenyekiti,makamu na mabaraza ya Vijana pamoja na wanawake Taifa yataanza kutolewa kuanzia tarehe 15 mwezi 11 mwaka huu hadi tarehe 22 mwezi 11 mwaka huu,katika wilaya zote,na akawata vijana wote kujitokeze ili kugombania nafasi hii yenye uwezo wa kukijenga chama hicho.
No comments:
Post a Comment