Tuesday, November 11, 2014

HII NAYO INAKUFAA USOME KUTOKA SERIKALINI LEO

 Na Karoli Vinsent

SERIKALI imesema idadi ya vijana wanaotumia kondom imeongeza kwa kiwango kikubwa tofautisha na miaka mingine,na kusema ongezeko hilo limesaidia kupunguza mambukizo mapya ya virus vya Ukimwi nchini.
       
           Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na  Mratibu wa Uzazi wa Mpango kitaifa kutoka wizara ya Afya nchini bwana Mouris Hiza,wakati wa semina kwa wadau mbalimbali wa mambo ya afya ambapo seminia hiyo iliyoandaliwa na Kampuni isiyo ya kiserikaliya DKT International inayoshugulika  kutoa elimu kuhusu uzazi wa Mpango,ambapo  alisema hali ya sasa ya matumizi ya kondom hususani kwa vijana imeongezeka kwa kasi.

          “Kiukweli hali ni inaridhisha sana na jitihada hizi za maongezeko ya matumizi ya Kondom kwa vijana imetokana na kazi nzuri iliyofanywa na Wizara ya Afya pamoja na Taasisi mbalimbali za kupambana na Virusi vya ukimwi,na hii imetokana na vijana wengi kutumia kondom katika kuzuia mimba na ukimwi nah ii ni jamba jema”alisema Hiza

          Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni  hiyo isio kuwa ya kiserikali ya DKT Davis Kambi alisema ni wakati umefika kwa serikali kutoa elimu kwenye kwa watanzania kuhusu umuhimu wa uzazi wa mpango kama Taasisi hiyo inavyofanya.


No comments: