Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Ripoti ya utafiti uliondaliwa na taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya TWAWEZA kumpa nafasi kubwa Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond, Edward Lowassa kwamba ndiye anayefaa kumrithi Rais anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2015 na kuwapiku wanasiasa wengine ikiwemo Waziri mkuu Mizengo Pinda na wengine ndani ya chama cha Mapinduzi CCM ,
Sasa Ripoti hiyo imeanza kupingwa na wadau mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi CCM,na kusema ripoto hiyo imejaa ubabaishaji mtupu wenye lengo wakuwadanganya watanzania kuwaamini kwamba viongozi hao ndio wanafaa kumbe sio kweli.
Akipinga Ripoti hiyo ya TWAWEZA waziwazi, ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Jannuary Makamba ambaye amesema hata utafiti wenyewe umejikitia sehemu moja tu tena mjini na haujafika hata katika visiwa na vya unguja na pemba na misingi hiyo inazidi kushusha hazi utafiti wenyewe.
Makamba ambaye ni Miongoni mwa wasaka urais kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi ambaye amejiapiza kufa na kupona kushika nafasi kumrithi Rais anayemaliza mda wake Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumza na Redio ya Magic Fm katika kipindi cha Morning Magic,
Ambapo alizidi kwenda mbali zaidi huku akionekana akimbeza Msaka Urais Mwenzake kutoka chama cha Mapinduzi CCM na mbunge wa monduri Edward Lowassa,na kusema inasikitika kuona mtu zaidi ya miaka kumi akiusaka urais na watanzania wanamjua leo nafasi yake imeshuka sana kupitia utafiti huo,
Makamba ambaye Vilevile ni kiongozi kijana kutoka ccm,aliendelea kusema CCM kinasifa 13 wakati wa kumteua mgombea wa urais ambazo ziliwekwa tangu mwaka 1985 ambapo sifa zipo wazi ikiwemo sifa za uadilifu,
Vilevile Makamba akatolea mfano 1995 ambapo wakati wa wakumtafuta mgombea kupitia CCM, walitumia sifa hizo na wakati huo walikuwepo wanasiasa maarufu,ila wakati wa kwenda Mkoani Dodoma na Wagombe hao maarufu wakataliwa na CCM na akachaguliwa mgombea ambaye ni ajulikani kabisa na akasema kuwa CCM haichagui kiongozi kutokana na Umaharufu kama aliyokuwa nao Lowassa.
Kwa upande wake mwandishi wa Habari kutoka Redio Mario Joseph mwalukusa alisema ripoti hiyo inamakosa mengi kwani imewaaangalia watu wa mijini tu na kuwaacha watu wavijini na akaongeza kuwa ni wazi kutakuwa na njama zinafanywa ili kumbeba mtu ambaye anarekodi za uchafu ili achaguliwe na watanzania
No comments:
Post a Comment