Meneja bidhaa wa kampuni hiyo EDWIN MGOA akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam |
Kampeni kubwa
inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania maarufu kama TIGO
WELCOME PACK mwishoni mwa wiki hii litakuwa mkoani mwanza ambapo wasanii
mbalimbali nchini Tanzania watatumbuiza katika tamasha litaklalofanyika mkoani
humo siku ya jumamosi.
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es
salaam meneja bidhaa wa kampuni hiyo EDWIN MGOA amesema kuwa kampeni hiyo ya
WELCOME PACK inayoendelea kwa muda wa mwezi mmoja sasa imekwisha fanyika kwa
mafanikio makubwa katika mikoa mingine huku akiitaja mikoa hiyo kuwa ni kagera,Kilimanjaro,arusha,iringa,Dodoma,na
mbeya ambapo imewapa fursa maelefu ya wateja wake kupata huduma zaa tigo kwa
karibu ikiwemo kufurushi cha WELCOME PACK.
FID Q akizungumza |
YOUNG KILLER MSODOKI atakuwepo siku hiyo ya Jumamosi |
Ameongea kuwa tamasha hilo limeandaliwa kwa ajili ya
kusherehekea huduma hiyo mpya mahususi kwa wateja wao na kwa safari hii tigo Tanzania
imeamua kwenda kutikisa jiji la mwanza baada ya kufanya vizuri katika mikoa
kadhaa nchini Tanzania.
Msanii kutoka kundi la origino komed akizingumza na wanahabari |
Baadhi ya wasanii watakaotikisa mkoani mwanza ni
pamoja na kindi maaruifu la vichekesho Tanzania ORIGINO KOMED,na wasanii kama
FID Q,YOUNG KILLER,pamoja na MWANA FA.ambapo kwa pamoja wameahidi burudani ya
aina yake siku hiyo ya tamasha.
Tamasha hilolitafanyika siku ya jumamosi kuanzia saa
6 mchana,ambapo kiingilio katika tamasha hilo ni kuwa na laini ya tigo tu.
Kampeni ya TIGO WELCOME PACK itakuwepo kwa miezi
mitatu ambapo misafara zaidi ya 70 ikiwemo basi la tigo la kidigital lenye
malengo ya kuwaelimisha wateja kuhusu huduma za tigo za kidigital
litatembea miji zaidi ya 70 na vijiji zaidi ya 100ndani ya mikoa 10
tofauti nchini Tanzania.
PICHA NYINGINE ZA MKUTANO HUO NA WANAHABARI ZIPO CHINI HAPO
No comments:
Post a Comment