JESHI LA POLISI LATOA TAHADHALI KWA WANAWAKE KUTOSHIRIKI KIMAPENZI NA WATU WASIOWAJUA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM LATOA TAHADHALI KWA WANAWAKE KUTOSHIRIKI KIMAPENZI NA WATU WASIOWAJUA
         
       Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la Dar es Salaa hususani wasichana kuwa makini na wanaume wanaowataka kimapenzi na baadaye kuwauwa na kutelekeza miili yao.


       Zimekuwepo taarifa juu ya kuwepo kwa wanaume wawili wanaoshawishi wanawake kuwa nao kimapenzi na baada ya muda huwauwa. Hivyo natoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la Dar es Salaam kuchukua tahadhali juu ya watu hawa maana huatarisha maisha yao au ya familia zao.

       Inaaminika watu hao huwashawishi akina dada au wanawake kwa jumla ili wawe nao kimapenzi huku wakiwasaidia kwa huduma mbalimbali za kimaisha na kisha kuwauwa.

         Natoa wito kwa wanawake wote kutokukubali kushawishiwa kirahisi na wanaume wasiowajua ambao wanataka kuwa nao kimapenzi na starehe kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuingia katika mtego mbaya na pengine hata kuyaweka maisha yao rehani.
Aidha, katika siku za hivi karibuni yameripotiwa matukio kadhaa ya mauaji ya aina hiyo ambapo kwa sasa wanawake wapatao sita tayari wamepoteza maisha. Haijafahamika madhumuni ya wauaji hao na huenda ni mambo ya ushirikina n.k.

       

Msako mkali unaendelea ili kuwabaini na Jeshi la Polisi Kanda Maalum linatoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutoa taarifa sahihi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya usalama ili kuwabaini na kuwakamata ili sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wahusika.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.