Tuesday, November 25, 2014

ESCROW--MAMA MARIA NYERERE AIBUKA MCHANA HUU,SOMA ALICHOWAAMBIA WANAHABARI NYUMBANI KWAKE

Mama  MARIA NYERERE ambaye ni mke wa baba wa taifa hili mwalimu NYERERE akizungumza na wanahabari muda huu nyumbani kwake jijini DAR ES SALAAM
Na karoli Vinsent

        SAKATA la Ufisadi wa zaidi ya Bilioni 400 kwenye Akaunti Tegeka Escrow iliyoko Benki kuu,lazidi kuwaibua watu mbalimbali Kupinga wizi huo ,baada ya leo Mama  Maria Nyerere kuibuka na kuzivaa mahakama pamoja na Bunge kwa kitendo chake cha kutumia kipengele cha sheria walizotunga wao kuwalinda wezi wanaliibia taifa mabilioni ya mapesa.

             Kauli hiyo ya mama Maria Nyerere ameitoa mda huu jijini Dar Es Salaam,wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini kutaka kufahamu kuhusu mwenendo wa nchi,ambapo Mama Nyerere alisema inashangaza sana viongozi wa leo ambao wanashindwa kumuenzi baba wa taifa kwa kuzidisha wizi wa mali za umma huku wakilindwa na sheria walizozitunga.
   
          “Yaani inasikitisha sana leo watu wanasogeza mali za umma kwenda kwenye mifuko yao huku tukishuhudia wengine hawana dawa kwenye hospitali,harafu tunaambiwa wezi hawa wanaofanya unyama huu wanalindwa na sheria,wakati leo unapita kwenye mitaa huku unamkuta mwizi ameiba kuku anachomwa moto,halafu anayeiba mali za umma analindwa na sheria sasa hii sheria ikoje jamani kwa sababu wtu wanakufa kwa kukosa dawa sheria haiwalindi hii ni vipi “ alihoji Mama Nyerere
    
             Mama Nyerere alizidi kuongea kwa uchungu huku akitaka hata kulia  alisema kwa sasa Viongozi wamekosa  maadili na kujikita kwenye wizi wa mali za umma kutokana na mifumo ya kimaadili ambayo imeanzia kwenye Familia na kupelekea hadi kwa watendaji wa serikali.
 Kuhusu Katiba iliyopendekezwa


Mama nyerere alisema katiba ni jambo jema katika nchi yeyote na akashanga kusikia leo watanzania wanagawanyika kisa katiba.
“katiba ni njia nzuri ya kulijenga taifa na tumeona hata nchi za Marekani wameifanyia marekebisho katiba zaidi ya mala 70,inakuwaje sisi leo katiba hii ndio itugawe kiasi hichi,leo katiba ndio itupeleke kwenye hali ya kupoteza umoja wetu,kiukweli nawaomba viongozi wa vyama vyote  vya siasa watoe tofauti zote kwenye jambo hili la katiba”alisema Mama maria Nyelele.
        
           Vyombo Vya Habari


Mama huyo wa Mwasisi wa Taifa hili  akusita kuvionya vyombo vya habari nchini na kuvitaka viache kutumia misamiati mibaya wakati wa kuripoti taarifa kwa wananchi na kuvitaka vitoe taarifa na misamiati ambayo kuundoa misuguano kwa jamii kwani itaweza kuwapunguzia hali ya ufanyaji kazi viongozi wa taifa.

No comments: