Tuesday, November 18, 2014

KUHUSU SYROSE BANJ KUFANYA FUJO KWENYE NDEGE,HII NDIO KAULI YA SERIKALI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhuDQZqGbU7ZCdjbw0jxqSzUzFbqTI4sNI6m8Ecs_emwwjKDRw_2tDt48PhS0s2qg8c2OyLNXNUTKePf30Orqx7IEHOUKq4cD0e81jrVXQuyX1fKFaEidujm_J8wghHI-nZK6rmZ-DOWS_e/s640/DSC04373.JPGNa Karoli Vinsent
           SERIKALI nchini imsema haiwezi kuingilia mgogoro unaoendelea kwenye Bunge la Afrika mashariki kati ya Mbunge wa Bunge hilo kutoka Tanzania Shyrose Banji na Wabunge wenzake kutoka nchi zengine zinazounda umoja huo wa Afrika mashariki na kusema kanuni za Bunge hilo, zinakaza serikali ya nchi yeyote kuingilia kazi au mambo ya bunge hilo.
        
           Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Siasa na Usalama wa kutoka Wizara ya Ushirikiano na Uhusiano Afrika Mashariki, Steven Mbundi wakati wa mkutano na waandishi ambapo Mbundi alisema kwa sasa serikali  ni kama imepigwa kufuli kuhusu sakata hilo kutokana na kanuni wazilijiwekea kwenye Bunge hilo.
    
             “Kwanza niseme hili sakata la mbunge wetu limekuwa likiandikwa sana kwenye kwenye magazeti na ukweli huku hivi sisi serikali hatuwezi kuingilia suala kwani kanuni za bunge hilo na utaratibi wake wa kuamua mamo na sisi serikali tutachukua hatua zaidi baada ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki atakapotua uamuzi”alisema Mbundi.
     
          Mbundi aliongeza kuwa Taarifa zinazoripotiwa kwenye mitandao ya kujamii na magazeti kuhusu Shyrose Banji kufanya Fujo kwenye Ndege walipokuwa wanakwenda kwenye Ziara ni za upande Mmoja ambazo hazijampa nafasi hata mwenyewe kujitetea na kusema ukweli wa Mambo utagundulika mara tu baada ya kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo kutoa majibu kwenye Kikao kichacho cha Bunge hilo.
    
           Na akatabainisha kuwa Serikali nchini ndipo itakapochukua hatua kwenye Jambo hilo.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Afrika Mashariki be Jocye Mapunjo alisema kwa sasa Muungano huo wa Afrika Mashariki unatakuwa na tija na wenye kubadilisha nchi zinazounda Umoja huo kuwa kwenye malengo ya maendeleo.
  
               “Kiukweli nawaomba watanzania wote watambue mchango wa ushirikiano huu,kwani duniani kote hata kwenye mataifa yaliyoendelea yamepiga hatua kutoka na mashirikiano kama haya,na ushiriano huu utakuwa na nafasi ya kuwabadilisha watanzia kuwa katika mipango mizuri ya maendeleo”alisema Be Mapunjo.
     
             Vilevile Be Mapunjo alisema kwa sasa wanakaribia kwenye mkutano mkuu wa jumuiya hiyo ambao utafanyika tarehe 30 Novemba mwaka huu huku Nairobi nchini kenya na kusema makutano huo utakuwa na mambo mengi yenye maendeleo.

        Jumuiya ya Afrika mashariki ni Muunganiko wa Nchi za Tanzania,Kenye,Uganda,Burundi na Rwanda ambapo Muunganiko licha ya kuwa na changamoto mbalimbali umeleta tija kwa wananchi wa Jumuiya hizi

No comments: