Saturday, November 8, 2014

SENTENS KALI TANO WALIZOIBUKA NAZO CHASO UDSM JUU YA VURUGU ZA MDAHALO WA WARIOBA

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kutoka chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA leo wameibuka na sentensi tano juu ya sakata la vurugu zilizoibuka wiki iliyopita wakati wa mdahalo uliokuwa unaendeshwa na taasisi ya mwalimu nyerere katika ukubi wa ubungo plaza ambapo kuliibuka vurugu kubwa na kufanya mdahalo huo kuvunjika.

Akilaani vurugu hizo mbele ya wanahabari leo jiini dar es salaam mwenyekiti wa CHASO Bwana JAMES MWANINYELA amesema kuna mambo matano ambayo wao kama wanafunzi wasomi wa Tanzania wanajiuliza uhusiana na vurugu hizo,mambo hayo ni kama yafuatayo---

1-Kwanza tunalaani vikali vurugu hizo

2-CHASO tunahoji ukimya wa menyekiti wa CCM TAIFA ndugu JAKAYA KIKWETE kwa baadhi ya viongozi wake na makada wa chama chake kwa kutishia kwa kutishia usalama wa viongozi wenye heshima kubwa nchini Tanzaniayani kama makamu wa rais mstaafu,na waziri mku mstaafu,jaji mkuu mstaafu,anahujumiwa na mwenyekiti taifa anakaa kimya  je raia wa kawaida itakuaje?nani yuko nyuma ya makonda?

3-Kwa kuwa Paul makonda ni katibu wa chipukizi wa UVCCM TAIFAjambo ambalo kimsingi ndio mtendaji mkuu CHASO UDSM tunataka kujua kama huo ndio utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya chama chake-CCM katika kulinda maoni hatamu ya katiba pendekezwa.

4-CHASO UDSM tunamtaka Paul makonda na baadhi ya UVCCM UDSM walioshiriki katika vurugu hizo wajitokeze hadharani na kuomba radhi kwa aibu kubwa waliolitia taifa.

5-Tunaomba watanzania kushiriki kikamilifu katika chaguzi za serikali za mitaana kukikataa Chama cha mapinduzi kwani sera zake zimeshindwa kuondoa maadui watatu yani ujinga,maradhi na umaskini na badala yake kimeongeza adui mwingine ufisadi.

Hizo ndio sentensi tano ambazo nimeona nikuwekee hapa mdau wangu
Mwenyekiti wa CHASO UDSM bwana JAMES MWANINYELA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam muda mfupi uliopita

No comments: