Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania Mussa Leonard Mdee akizungumza na wanahabari muda mfupi uliopita jijini Dar es salaam mapema leo |
Na Karoli Vinsent
SERIKALI imepewa siku saba kuhakikisha wanafunzi wa elimu ya Juu waliokosa mikopo kwa mwaka huu wanashughulikiwa na kupewa mikopo,kinyume na hapo wanafunzi wametangaza kutumia njia nyingine kali ikiwezekana kuandamana na kufanya Migomo ili kushinikiza nusu ya wanafunzi masikini waliokosa mikopo wanapewa ili waweze kuendelea na masomo ya elimu ya Juu.
Akitangaza Uamuzi huo mkali Leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari,Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania Mussa Leonard Mdee ambapo amesema wamefikia maamuzi hayo kutokana na kushangazwa na kitendo cha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuwanyima mikopo wanafunzi 28037 kati ya 58307 waliomba mikopo katika mwaka wa Masomo 2014-2015.
“Hali hii ni mbaya sana miongoni mwa wanafunzi waliotarajiwa kujiunga na Elimu ya Juu,ambapo mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 28,037wameshindwa kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo kutoka bodi ya mikopo nchini,ingawa wanafunzi wamefaulu kujiunga na Elimu ya juu na wanavigezo vyote vyenye kukidhi ya kupata mikopo huku ukizingatia wanafunzi hawa ni yatima hawana Baba wala Mama harafu leo hawajapewa mkopo”alisema Mdee.
Edward maclein mmoja wa wanafunzi aliokosa mikopo hiyo akitoa malalamiko mbele ya wanahabari jijini Dar es salaam leo |
Mdee alizidi kusema Jumuiya hiyo hajarizika na Majibu aliyoyatoa Waziri mkuu Mizengo Pinda Bungeni alipokuwa anajibu Swali aliloulizwa na Mbunge wa kigoma Kusini Zitto Kabwe aliyetaka kura za Maoni za kupitishwa katiba iliyopendekezwa isitishwe na Fedha ambazo zimetengwa kwa ajiri ya kazi hiyo,zipelekwe kwa wanafunzi waliokosa mikopo,ambapo waziri huyo mkuu alisema hawawezi kuhairisha kura ya maoni na kusema madai ya wanafunzi waliokosa mikopo wanashughulikiwa na wizara ya Fedha.
“Hii kauli ya waziri mkuu inatushangaza sana kwani kujisajili kwa wanafunzi hawa wa mwaka wa kwaza kulikoma tangu mwezi octoba katikati na sasa ni mwezi novemba,akitambua watoto hawa masikini mpaka sasa wako mitaani wakiwa hawajui hatma yao ,harafu anatoa majibu yasiyokuwa na muda wa utekelezaji yaani majibu haya ni ya kisiasa”aliongeza Mdee
Aidha, mdee alisema TAHLISO kwa kuonyesha inawajali wanafunzi basi inatoa siku saba kamili kwa serikali kutoa fedha hizo kwa wanafunzi waliokosa mikopo na wawe chuoni na kusema kuwa wanafunzi hawa wamechelewa kidogo masomo kwani yameanza tangu octoba,2014 na wakaitaka serikali kutoa mwongozo wa wanafunzi na kupolekewa vyuoni hata kama watakuwa wamechelewa vyuoni kwa waraka maalum.
Vilevile TAHLISO waliongeza kuwa siku saba zikiisha bila utekelezaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupewa mkopo,wataomba uungwaji mkono na Asasi za Kiraia,Mashirika na haki za binadamu,wazazi na walezi na watanzania wote mpaka wakulima kuandaa kuchukua maamuzi magumu ili kushinikiza wanafunzi waliokuwa mitaani ambao wameshindwa kwenda chuo kikuu kutokana na kukosa mikopo wapewe fedha hizo.
Kwa upande Edward Maclean ambaye ni mwanafunzi yatima alinyimwa fedha na serikali,alisema anashindwa kuelewa hatma yake ya masomo huku akizingatia hana baba wala mama.
“Kusema kweli mimi ni yatima sina baba wala mama,nimesoma kwenye shule za kata mpaka namaliza kidato cha sita,leo nimechaguliwa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) naambiwa sina mkopo kutokana na serikali kutokuwa na fedha,sijui mimi niende wapi”alihoji Maclean huku akitokwa na machozi
No comments:
Post a Comment