Tuesday, November 25, 2014

TIGO PESA YAREJESHA TENA FAIDA YA SHILING BILION 3 KWA WATEJA WAKE

         Tigo imetangaza leo kwamba imetoa malipo yake ya kwanza ya kila robo mwaka ya kiasi cha shilingi bilioni 3 (dola milioni 1.8) kwa wateja wake wa Tigo Pesa. Mgao huu ni wa kwanza kati ya awamu nne za malipo zinazotarajiwa kufanyika kila mwaka.


      Malipo haya yanafanyka miezi mitatu baada ya kampuni hiyo kulipa kiasi cha shilingi bilioni 14.25 (dola milioni 8.64) ambacho kilikuwa kimelimbikizwa katika mfuko wa fedha ya akaunti ya Tigo Pesa, malipo yaliyoifanya Tigo kuwa kampuni ya simu ya kwanza duniani kuwagawia faida watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa simu za mkononi. Tigo Pesa ina jumla ya watumiaji milioni 3.6.

      Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez alisema, “Hii duru ya pili ya kutoa gawio ni udhihirisho tosha wa muendelezo wa kampuni yetu katika kuwanufaisha wateja na kuboresha maisha ya Watanzania. Malipo haya yanaenda kwa kila mtumiaji wa Tigo pesa wakiwemo mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na watumiaji wa kawaida wa huduma hii. ”

      “Gawio la kwanza lilikuwa kubwa zaidi kwa sababu faida ilimbikizwa kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu na nusu ikilinganishwa na malipo haya ya pili ambayo yanatokana na malimbikizo ya faida ya fedha zilizohifadhiwa katika mifuko ya benki za kibiashara kwa muda wa miezi mitatu t kutoka Julai hadi Septemba 2014,” alisema Meneja Mkuu huyo.

        Gutierrez alieleza kwamba, kama ilivyokuwa hapo awali, malipo wanayopata wateja awamu hii yanatokana na salio lao la kila siku kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. Hii ni kwa wote; mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na watumiaji wa kawaida.   

Mgao unaofuata wa mwezi Oktoba mpaka Desemba 2014 utalipwa mwezi Februari 2015.

No comments: