ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY
TAARIFA KWA UMMA.
IMERIPOTIWA LEO KUPITIA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KATIKA KILE KINACHOTAJWA NI MGOGORO WA KISIASA NDANI YA CHAMA KATI YA WANAOJIITA WAASISI WA CHAMA NA VIONGOZI WAKUU WA CHAMA NA KUPELEKEA KUTOA TAMKO LA KUMSIMAMISHA KATIBU MKUU NA MUHASIBU WA CHAMA.
IFAHAMIKE KWAMBA BAADA YA CHAMA KUPATA USAJILI KIMEFANYA VIKAO VYA KAMATI KUU VITATU NA PIA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU KIMOJA VIKAO VYOTE HIVYO VIMEJADILI MIKAKATI NA MAENDELEO YA CHAMA HAKUNA KIKAO KILICHOJADILI MGOGORO NDANI YA CHAMA KWA SABABU HAKUNA MGOGORO.
HIVYO BASI KATIBU MKUU NA MUHASIBU HAWAJASIMAMISHWA NA KIKAO CHOCHOTE CHA CHAMA.
KUHUSU NDUGU LEOPOLD MAHONA AMBAYE NI NAIBU KATIBU MKUU BARA NA GREYSON NYAKARUNGU AMBAYE NI MWENYEKITI WA NGOME YA VIJANA KUENDESHA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI.
MKUTANO HUO HAUKUWA NA BARAKA ZA CHAMA LAKINI KWA KUWA ACT TANZANIA TUNAAMINI KATIKA DEMOKRASIA MALALAMIKO YAO TUMEYAPOKEA NA TAMKO LAO TUNALO TUTALIWASILISHA KTK VIKAO VYA CHAMA NA TUNAAMINI VIKAO VYA CHAMA VITATOA MAELEKEZO BORA YENYE KUKIIMARISHA CHAMA NA KUONGEZA MSHIKAMANO NDANI YA CHAMA.
KWA SASA KATIBU MKUU NA KATIBU WA FEDHA NA RASILIMALI WANAENDELEA NA MAJUKUMU YA UJENZI WA CHAMA HASA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA PROGRAM ZA CHAMA ZILIZOPITISHWA NA KIKAO CHA KAMATI KUU HIVI KARIBUNI.
AIDHA MAMBO YOTE YANAYOLALAMIKIWA YAMEPITISHWA NA VIKAO HALALI VYA CHAMA NA MIHUTAASARI IPO OFISINI KWA KATIBU MKUU HIVYO BASI TUNAWATAKA VIONGOZI WA MATAWI,KATA,MAJIMBO,MIKOA NA WANACHAMA WOTE KUWA WATULIVU NA KUENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO MKAKATI WA KUKIPATIA MAFANIKIO CHAMA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA,VIJIJI NA VITONGOJI.
ACT-TANZANIA TAIFA KWANZA LEO NA KESHO.
IMETOLEWA NA IDARA YA MAWASILIANO NA UENEZI TAIFA
No comments:
Post a Comment