Tuesday, November 4, 2014

VURUGU MDAHALO WA WARIOBA--WANAHARAKATI WACHARUKA,SOMA KILICHOZUNGUMZWA MUDA HUU JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari muda huu katika ofisi za makao makuu ya kituo hicho kijitonyama jjni dar es salaam,kushoto kwake ni  mkurugenzi msaidizi wa JUKATA ndugu HEBRONI MWAKAGENDA
Ikiwa ni siku kadhaa kupita tangu tukio la kufanyiwa fujo kwa mdahalo ulikuwa unafanyka jijini Dar es salaam chini ya mwenyekii wa tume ya mabadiko ya katiba Tanzania jaji JOSEPH SINDE WARIOBA, asasi mbalimbali  za kiraia wameibuka na kauli nzito ya kulaani kitendo hicho ambacho wamedai kuwa kinafedhehesha taifa.

Wakizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam wanaharakati hao wakIongozwa na mkurugnzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA wamesema kuwa kitendo cha kuvuruga mdahalo huo ni kitendo cha kulaaniwa na kila mtanzania mpenda haki na si kitendo kizuri katika mchakato wa kupata katiba ya Tanzania. 
Wanahabari wakiwa wanafwatilia kwa umakini 

          “ndugu wanahabari kitendo cha kufanya vurugu katika mdahalo wa juzi kinapaswa kulaaniwa na kukemewa na kila mwananchi mwenye mapenzi mema na taifa la Tanzania na hasa viongozi wananchi wenye dhamana yakulinda na kutetea democrasia na amani tuliyo nayo.amesema bi HELLEN.

           Aidha amesema kuwa vurugu hizo zimeonyesha kuwa zina lengo la kuwatisha wanachi wasijadili katiba waitakayo kwa muskatabali wan chi yao,ambapo amesema kuwa ni lazima kitendo hiki kikemewe na kila mtanzania ili kuweza kuweka dmocrasia ya kweli katia kutoa maoni ya katiba ya Tanzania.
         Katika hatua nyingine wanaharakati hao wamvitaka vyombo vya  sheria kuhakikisha kuwa wanawatia mbaroni vijana wote walioonekana kuanzisha vurugu hizo juzi katika mdahalo huo kwani kuna njia nyingi za kuwakamata ikiwa ni pamoja na kutiza mikanda ya video ambayo imerekodiwa aidha na uongozi wa ukumbi huo au wanahabari. 
 mkurugenzi mstaafu wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA bi ANANILEA NKYA akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam
           Akizungumza na wanahabari katika mkutano huo mkurugenzi mstaafu wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA bi ANANILEA NKYA amesema kuwa kuna kila dalili kuwa kikundi kilichofanya fujo juzi ni kikundi ambacho kuimeandaliwa kwa ajili ya kuvuruga mchakato huu wa katiba hivyo amewataka watanzania kuwa makini na kikundi hicho kwani sio kikundi chenye malengo mazuri kwa watanzania.

        Wakizungumzia swala la kufanyika midahalo ya katiba ikiwa bado muda wa kuipigia kampeni katiba pendekezwa haujatangazwa mkurugenzi wa SIKIKA IRINET KIRIA amesema kuwa haki ya kutoa maoni ni haki ya kila mtanzania na hakuna mtu ama sheria inayomkataza mtu kutoa maoni yake kuhusu mambo nyeti ya watanzania kama swala la katiba.
Mkurugenzi wa SIKIKA IRINET KIRIA  akifafanua jambo katika mkutano huo

         Tukio la kufanyika kwa vurugu katika mdahalo huo lilitokea jumapili mchana katika ukumbi wa ubungo plaza jijini dar es salaam ambapo mdahalo ulikuwa umeandaliwa na taasisi ya mwalimu nyerere ulivunjika baada ya vijana kadhaa kuanzisha vurugu katika ukumbi huo na kupelekea watu kadhaa kupigana na hata mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji WARIOBA kunusurika kupigwa.


No comments: