Tuesday, November 4, 2014

HABARI HII NAYO HUTAKIWI KUIKOSA

1
Rais wa tuzo za TWA Irene Kiwia akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya Serena  jijini Dar es salaam wakati akielezea maandalizi ya tuzo hizo kwa mwaka huu wa 2014, Katikati ni Mwenyekiti wa tuzo za TWA mama Sadaka Gandi na kulia ni Hellen Kiwia katibu TWA.
2
Mwenyekiti wa tuzo za TWA mama Sadaka Gandi  akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akielezea maandalizi ya tuzo za Mwanamke za TWA, Kulia ni Rais wa tuzo za TWA Irene Kiwia



Taasisi ya Shirika la kijamii TanzaniA Women of Achievement (TWA) leo  wamezindua rasmi Tuzo za Wanawake wenye MafanikioTanzania ambazo zitafanyika tarehe 7/3/2015 kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake, likiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake ambao wamechangia maendeleo Tanzania katika nyanja tofauti.
Rais wa shirika la Wanawake Wenye Mafanikio Bi. Irene Kiwia alisema “ Lengo la TWAA ni kusheherekea mafanikio ya wanawake hawa na kazi wanazozifanya kwenye jamii kupitia nyanja tofauti ndani ya Tanzania.  Vigezo mbalimbali vitatumika katika kuwachagua  kama vile utofauti waliouonyesha katika jamii zao, jinsi gani wameweza kuwavutia na kuwashawahi watu wengine, na jinsi gani wameweza kuwagusa na kuwafikia watu tofauti tofauti.”
Bi Kiwia alisema kwamba “ Tuzo hizi pia zitaenda sambamba na na mafunzo ya kujenga uwezo wa wasichana viongozi katika nyanja tofauti  walio kati ya umri wa miaka 18-27 kutoka mikoa yote ya Tanzania ambayo yatachukua wiki 6. Wasichana hao watakutanishwa na wanawake wanaofanya vizuri katika biashara, kazi za jamii na idara tofauti kwa ajili ya kupewa motisha an kujifunza. Mategemeo yetu ni kuwa baada ya mafunzo haya wasichana  wataenda kuwa  chachu ya mabadiliko mikoani kwao na kuwafundisha wenzao wengi ili kusambaza  mori wa maendeleo an mabadiliko kwa wasichana wadogo nchini kote.
Mwenyekiti wa TWAA, Mrs. Sadaka Gandhi alisema “suala la uwezeshaji kwa wanawake linapewa kipaumbele duniani kote, tuzo hizi zitaonyesha uwezo na ugunduzi  wa wanawake katika sehemu tofauti. Tunaamini kuwa wale wote watakaoshiriki  watakuwa chachu ya mabadiliko kwa wasichana kutoka vijijijini, wafanyabiashara na wanawake wengi chini Tanzania”.
“Katika kipindi cha miezi mitatu, tunaomba watu mbalimbali wajitokeze kuchagua wanawake ambao wanafanya vizuri katika fani zote kuanzia mfanyabishara mwenye jitihada kubwa, mwalimu wa namna ya kipekee na hata mtu ambaye ameweza kuleta mabadiliko muhimu katika jamii yake.” Alimalizia Mrs. Gandi.
Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni  sanaa na utamaduni, ujasiriamali, elimu, afya, sayansi na teknolojia, kilimo, ustawi wa jamii, michezo, umma, mshiriki wa mafanikio mwenye umri mdogo, mwanamke aliefanya vizuri ndani ya mwaka mzima na mwanamke aliefanya vizuri katika maisha yake.
Washiriki wanaweza kujipendekeza ama kupendekezwa la shirika kupitia www.twa.or.tzinfo@twaa.or.tz kabla ya tarehe 30 Januari 2015. Washiriki lazima wawe ni wakazi wa Tanzania ambao kazi zao zimefanyika Tanzania. Washiriki watatu katika kila kipengele watatangazwa kabla ya siku ya sherehe ya Tuzo za Wanawake Wenye Mafanikio mwezi Machi mwakani.
Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello,  Dk. Marcelina Chijoriga – kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana. Innocent Mungy – Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.
Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, TheAmerican People, DTP, UN Development Partners Gender Group, UNFPA, UNESCO, UN Women,TBL, Multichoice, Africa Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip CompanyRBP, Clouds FM, Thinline, Costech, Kairuki Hospital, ZARA Tours, Serena Hotel, Tigo, African Lynx Investment, EATV na EA radio na Frontline Porter Novelli

No comments: